GIMBI MASABA ARUDISHA FOMU KUTAKA AWE MWENYEKITI KAMILI WA CHADEMA KANDA SERENGETI BAADA YA KUKAIMU NAFASI HIYO KWA VIPINDI VIWILI


GIMBI MASABA ARUDISHA FOMU KUTAKA AWE  MWENYEKITI KAMILI WA CHADEMA KANDA SERENGETI BAADA YA KUKAIMU NAFASI HIYO KWA VIPINDI VIWILI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

KAIMU Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti kwa Vipindi Viwili sasa Gimbi Masaba,amerudisha Fomu ya kugombea Rasmi Uenyekiti wa Chadema Kanda hiyo ili awe Mwenyekiti kamili, katika Uchaguzi wa ndani wa Chama hicho wa kuwania nafasi za uongozi kikanda,ambao utafanyika hivi karibuni.
Zoezi la urudishaji Fomu kugombea nafasi za uongozi Kikanda ndani ya Chama hicho mwisho ni leo Aprili 22,2024, na baada ya hapo Chama kitakaa ili kupitisha Rasmi majina ambayo yatagombea nafasi za uongozi ngazi ya Kanda.

Gimbi akizungumza mara baada ya kurudisha Fomu hiyo,amesema ni wakati wake sasa wa kuwa Rasmi Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti, ambayo inahudumu Mikoa Mitatu ya Simiyu, Mara na Shinyanga, sababu amekaimu nafasi hiyo kwa vipindi viwili hadi sasa na anauzoefu mkubwa.
“Baada ya kukaimu nafasi hii ya Uenyekiti Chadema Kanda ya Serengeti kwa vipindi viwili sasa, nimekaa na kujitathimini ni kaona ni vyema nichukue fomu ya kugombea ili niwe Mwenyekiti kamili, sababu uzoefu ninao wa nafasi hii na uwezo ninao,”amesema Masaba.

“Kwa sasa siwezi kuzungumza mengi ambayo nimefanya katika nafasi hii ya kukaimu Uenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti, nazani kila mtu anafahamu nimefanya nini, ila nitazungumza zaidi pale Chama changu kitakapopitisha jina langu kugombea rasmi nafasi hii ya Uenyekiti na kuanza Kampeni, ndipo nitaelezea vitu ambavyo nimefanya,”ameongeza.
Kaimu Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti Wiliamu Shayo, amesema katika Kituo cha Shinyanga wagombea waliorudisha Fomu ni 13, ambapo nafasi ya Uenyekiti amerudisha Gimbi Masaba,James Mahagi na Emmanuel Ntobi, huku nafasi ya Umakamu Mwenyekiti amerudisha Mtu Mmoja Wiliamu Ademba.

Amesema kwa upande wa nafasi ya Mwekahazina wamerudisha Fomu watu watatu, Mwenyekiti Baraza la Wanawake (BAWACHA) Wawili, na Makamu wake wawili, Baraza la Vijana (BAVICHA) wawili, na Baraza la Wazee Mmoja, na kwamba zoezi la urudishaji Fomu lilikuwa mwisho leo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti Gimbi Masaba, (kulia) akirudisha Fomu ya kugombea Rasmi nafasi ya Uenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti baada ya kuikaimu nafasi hiyo kwa vipindi viwili sasa na kutaka awe Mwenyekiti kamili.
Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti Gimbi Masaba, akizungumza mara baada ya kumaliza kurudisha Fomu ya kugombea Rasmi nafasi ya Uenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti baada ya kuikaimu nafasi hiyo kwa vipindi viwili sasa na kutaka awe Mwenyekiti kamili.
Wiliamu Patrobas Odemba akizungumza mara baada ya kumaliza kurudisha Fomu ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti.
Jackson Tungu akizungumza mara baada ya kumaliza kurudisha Fomu ya kugombea nafasi ya uwekahazina Chadema Kanda ya Serengeti.
Viongozi mbalimbali wa Chadema wakiwa kwenye Ofisi za Chadema Kanda ya Serengeti.
Viongozi mbalimbali wa Chadema wakiwa kwenye Ofisi za Chadema Kanda ya Serengeti.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464