MADIWANI SHINYANGA WALALAMA VITUO VYA KUCHOTA MAJI “MAGHATI”VYASITISHA HUDUMA KWA WANANCHI
MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wamelalamikia Vituo vingi vya kuchota Maji (Maghati) katika maeneo mbalimbali havitoi huduma hiyo,huku vingine vikiwa vimefungwa kabisa na kusababisha wananchi kukosa huduma ya Maji,huku likielezwa tatizo ni madeni kutokana na wasimamizi wa vituo hivyo ambao ni wauzaji kutoroka na fedha za mauzo.
Wamebainisha hayo leo Aprili 30,2024 kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo tatu ya mwaka kuanzia Januari hadi Machi wakati wa Ajenga ya Taarifa ya Mkurugenzi kutoka kwenye Taasisi za Serikali, kipindi cha uchangiaji wa Taarifa ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).
Wamesema Maghati mengi kwa sasa hayatoi huduma ya maji kwa wananchi huku mengine yakiwa yamefungwa, na kusababisha wananchi kukosa maji.
Mmoja wa Madiwani hao Diwani wa Kitangili Mariamu Nyangaka, amesema wanashindwa kuelewa sababu ambazo zimesababisha Maghati hayo ya Maji kushindwa kutoa huduma kwa wananchi na hivyo kutaka majibu.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko naye amehoji kutaka kujua ni sababu zipi hasa ambazo zimesababisha Maghati ya Maji kutoa huduma kwa wananchi, na kwamba SHUWASA wanaposema sababu ni madeni wanashindwa kuelewa kutokana na watu ambao waliweka kusimami mauzo ya maji na wakatoroka na fedha hizo waliwaweka wenyewe.
"SHUWASA mnapotuambia kwamba Maghati hayatoi Maji sababu ya Madeni tunashindwa kuelewa,hebu tupeni ufafanuzi mzuri kwanini Maji hayatoki,sababu taarifa tulizonazo watu ambao mliwaweka wenyewe kuuza Maji ndiyo wametoroka na fedha za mauzo,nani watu wenu wenyewe,sasa kwanini watu hawapati maji," amehoji Masumbuko.
Naye Mkurugenzi wa SHUWASA Mhandisi Yusuph Katopola, akitoa majibu kwenye Baraza hilo,amesema Maghati ya kuchotea Maji yamekuwa na Changamoto ya usimamizi, kwa watu kukosa uaminifu na kutumia fedha za mauzo ya maji.
Amesema sababu kubwa ambayo imesababisha Maghati mengi kusitisha utoaji wa huduma ya Maji ni Madeni, kutokana na wasimamizi wake kutolipa bili za maji, na kwamba kwa sasa wanachokifanya ni kuangalia utaratibu wa kuweka Mita za Maji za Malipo ya kabla.
Ametaja sababu nyingine Maghati ya Maji kufungwa, kwamba Matumizi ya Maji kwa wananchi yamekuwa madogo, sababu baadhi wameshavuta Maji majumbani mwao, na hivyo kusababisha mauzo ya maji kuwa chini.
"Watu ambao tunawaweka SHUWASA kusimamia mauzo ya maji hua tunawalipa asilimia 20 ya ukusanyaji wa Mapato, sasa kama Mtu anauza Maji kwa Mwezi Sh.Elfu 20 ina maana alipwe Sh.Elfu 4, kitu ambacho wengi hua hawakubali ndiyo maana uaminifu unakuwa mdogo,"amesema Mhandisi Katopola.
Aidha,amewaomba Madiwani kwamba kwenye maeneo ambayo Maghati ya Maji yanahitaji zaidi kwa wananchi wawasiliane na SHUWASA, ili huduma ya Maji irejeshwe licha ya kuwapo kwa Madeni hayo, pamoja na kuwasaidia kupata watu waaminifu ambao watasimamia mauzo ya maji.
Kikao hicho cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga,kimepokea na kujadili taarifa mbalimbali,zikiwamo za Kamati ya kudhibiti Ukimwi,Mipango Miji na Mazingira,Uchumi Afya na Elimu, pamoja na Fedha na Utawala.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha Baraza.
Kikao cha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga kikiendelea.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga likiendelea.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga likiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464