SHIRIKA lisilo la kiserikali la TCRS ambalo linajihusisha na utunzaji wa mazingira na kutoa misaada kwa watu walioathiriwa na majanga mbalimbali, limetoa msaada wa nguo kwa wakazi 419 sawa na kaya 51 walioathiriwa na mafuriko ya maji ya mvua yaliyotokea tarehe 15/02/2024 na kuvikumba vijiji vitatu vya Mwamashele, Isagala na Igaga vilivyoko katika kata ya Mwamashele Wilayani Kishapu.
Wafanyakazi wa Shirika la TCRS wakikabidhi Nguo kwa Waathirika wa Mafuriko.
Akitoa taarifa ya msaada huo kwa wananchi hao Afisa miradi wa Shirika la TCRS Kishapu Dkt. Oscar Rutenge amesema msaada huo wa nguo uliotolewa umepata uwezesho kutoka kwa wadau mbalimbali wanje akiwemo Pst. Yokota wa nchini Japan na Shirika la Canadian Lutheran World Relief (CANADA)nguo zenye thamani ya Sh.milioni 5,545,000.
Afisa Miradi Shirika la TCRS Kishapu Dkt. Oscar Rutenge (kulia) akiwa na Wataalamu wa Halmashauri ya Kishapu.
Aidha amewataka wananchi hao kutunza nguo hizo ili ziwasaidia kupata nafuu ya maisha wakati huu wa kurudisha hali ya familia zao.
Wafanyakazi wa Shirika la TCRS wakikabidhi Nguo kwa Waathirika wa Mafuriko.
Miza John ni Afisa Mtendaji wa Kijiji ncha Mwamashele amesema wananchi wengi walioathiriwa na mafuriko hayo walibaki bila chakula na baadhi ya mifugo Ng’ombe Mbuzi na Kuku walikufa huku akitumia muda huo kuwataka wananchi hao kutumia fedha watakazopata baada ya kuuza mavuno kujenga nyumba imara katika makazi yao.
Mratibu wa Maafa Wilaya ya Kishapu bwana Robert Mhina amesema toka mafuriko hayo yatokee mashirika mengi yamekuwa yakijitokeza kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwemo chakula, mbegu, dawa za kutibu maji na sasa TCRS kwa kushirikiana na baadhi ya wadau kutoka nje ya nchi liliwemo shirika la Canadian Luthetan World Relief (CANADA) na Pst Yokot wa Japan wamekuja na msaada wa nguo kwa makundi yote ya Wanaume, Wanawake na Watoto.
Mratibu wa Maafa Wilaya ya Kishapu bwana Robert Mhina akizungumza na Waathirika wa Mafuriko.
Akitoa msisitizo kwa waathirika wa mafuriko Mrati bu wa maafa (W) Kishapu bwana Robert Mhina amewataka wananchi wa Wilaya ya Kishapu kutunza chakula cha kutosheleza wakati huu wa mavuno ili kuwasaidia kurudisha hali za familia zao zilizotetereka baada ya kupoatwa na janga huku akiwataka kujenga nyumba imara zinazohimili misukosuko ya mvua na upepo mkali.
Omary zengo kwa niaba ya wananchi wa vijiji vilivyoathirika na mafuriko hayo ameshukuru kwa msaada wa nguo kutoka TCRS na kuyaomba mashirika menine, Serikali na wadau wengine kuendelea kuwasaidia ili warudi katika maisha ya kawaida baada ya kupatwa na janga la mafuriko.
Omary zengo Muathirika wa Mafuriko akisaini makabidhiano ya nguo.
Jioseph Petro Masanja ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwamashele amelishukuru Shirika la TCRS pamoja na wadau wanje ya Nchi ambao ni Canadian Luthetan World Relief (CANADA) na Pst Yokot wa Japan kwa msaada huo kwa wananchi na kuwataka wasichoke kusaidia watu punde wanapiopatwa na majanga mbalimbali.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI TUKIO LA KUKABIDHI NGUO ZA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KISHAPU👇
Wafanyakazi kutoka Shirika la TCRS wakiwa na Kiongozi wa Serikali wilayani Kishapu wakiteta Jambo
Wafanyakazi wa Shirika la TCRS wakiwa na viongozi mbalimbali wa Serikali kwenye zoezi la ugawaji nguo kwa Waathirika wa Mafuriko Kishapu.
Zoezi la Ugawaji Nguo likiendelea kwa Waathirika wa Mafuriko wilayani Kishapu.

Waathirika wa Mafuriko wakisaini baada ya kumaliza kukabidhiwa nguo.

Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha ya pamoja ikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464