HALMASHAURI YA SHINYANGA KUHUISHA MABARAZA YA WATOTO,KATA YA LYAMIDATI KUWA KANDA MAALUM DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI

HALMASHAURI  YA SHINYANGA  KUHUISHA MABARAZA YA WATOTO,KATA YA LYAMIDATI KUWA KANDA MAALUM DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI.

Wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA  wakiwa katika kikao.

Na
Estomine Henry na Stella Homolwa,Shinyanga Press Club Blog

Kamati ya ulinzi na usalama wa wanawake na watoto (MTAKUWWA) ya Halmashauri ya wilaya  ya Shinyanga  imeazimia kuhuisha mabaraza ya watoto  katika shule za msingi na sekondari ili kuongeza juhudi za mapambano dhidi ya ukatili.

Kamati hiyo ya MTAKUWWA ya Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ilipitisha azimio hilo aprili 12 mwaka huu katika kikao cha 4 cha robo mwaka kwa ajili  tathimini ya hali ya ukatili dhidi ya wanawake  na watoto ,ambapo  watendaji wa serikali,viongozi wa dini,baraza la watoto na asasi za kirai wameshiriki kikao hicho.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Kisena Mabuba,alisema serikali ilitoa agizo la uanzishaji na usimamiaji wa mabaraza ya watoto kupitia MTAKUWWA kwa shule zote ili kupambana na ukatili dhidi ya watoto kwa kuimarisha usalama wao.

"Nitatoa maelekezo kwa waalimu wa malezi na nitapita kila shule kuongea na wajumbe wa mabaraza ya watoto kuona kama watendaji wa serikali wanashiriki kusimamia mabaraza haya,hili jambo tulichukulie kwa umuhimu mkubwa na tujitafakari kama mamlaka na hakikisheni mabaraza yote yanahuhishwa na kufanya kazi"amesema Mabuba.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Kisena Mabuba akizungumza katika kikao cha  kamati ya ulinzi na usalama wa wanawake na watoto.
Halmashauri  hiyo ilifikia azimio hilo baada ya hoja kutoka baraza la watoto kulalamika kutopata ushirikiano  kutoka kwa walimu wa malezi.

Mwenyekiti wa baraza la watoto Halmashauri  ya wilaya ya Shinyanga, Amina Khamis amesema mabaraza ya watoto hayapati ushirikiano kutoka kwa walimu wa malezi na kuyafanya kufa kila wakati.

"Walimu wa malezi wanatuangusha kwa kutotupa ushirikiano na tunajikuta pekee yetu hadi inabidi nitumie mbinu ya kuwapa watoto wenzangu zawadi ili washiriki na kunisikiliza"Amesema Amina Mwenyekiti baraza la watoto Halmashauri ya Shinyanga na kuongeza kuwa

"Mabaraza ya watoto yanakufa iwapo viongozi wanapohitimu shule na kutoandaliwa kwa viongozi wengine mapema ili kusimamia mabaraza haya"amesema Amina
Mwenyekiti wa baraza la watoto Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Katibu baraza la watoto Shinyanga,Amina Khamisi akitoa hoja juu ya kufa kwa mabaraza ya watoto.
Wawakilishi wa baraza la watoto wakisikiliza 
Aidha,Mabuba amesema Kata ya Lyamidati ina changamoto za matukio mengi ya ukatili na inahitaji nguvu ya wadau wote kuisaidia jamii na ni vema iwe kanda maalum kwa jicho la ziada la nguvu ya  wadau na serikali.

"Naomba muweke macho yenu kwa Kata ya Lyamidati ili kuzuia vitendo vya ukatili,hili liwe eneo la kivita tuifanye kuwa Kanda maalum kuna shida kubwa pale kwani hata jamii inaunga mkono uovu kwani kuna hata baadhi ya watoto hawaendi shule na wanajamii wanuunga mkono na matukio ya mimba na ndoa za utotoni ndo inaongoza"amesema 

Kwa upande mwingine,Wadau watekelezaji wa mradi wa ukatili wameshauri watendaji wa serikali kufahamu kwa upana matokeo ya wadau na  kuyaeleza na kujifunza kupitia utafiti na uzoefu wa wadau mbalimblai  katika utakelezaji wa afua za ukatili kwa halmashauri hiyo.
"Haya ni matokeo  makubwa kwa  Halmashauri   kutenga bajeti kila mwaka kwa masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto" Groly mbia,Mratibu wa Mfuko wa Wanawake Tanzania.
Mratibu wa Mfuko wa wanawake Tanzania, Groly Mbia ,akizungumza namna WFT-T  inavyoshirikiana na Halmashauri ya wilaya Shinyanga katik kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Wajumbe wakisikiliza wakifatilia hoja za kikao
Mratibu wa shirika la YWL( Young Women Leadership) akiwasilisha hoja juu ya mabaraza ya watoto.
Mwakilishi wa Shirika la GCI(Green community Initiative) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ukatili unalenga afua ya malezi na stadi kazi kwa watoto.
Meneja wa Redio faraja fm,Simeo Makoba  akiwasilisha taarifa utekelezaji wa mradi wa ukatili kupitia redio jamii.
Mratubu wa klabu ya waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga,Estomine Henry akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ukatili wa klabu ya waandishi habari.
Mratibu wa shirika la YAWE ,Moshi Jilalage  aliwasilisha hoja wakati wa kikao.
Mtendaji wa kata ya nyamalogo akiwasilisha hoja wakati wa kikao.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464