ILEJE NA MKAKATI WA MALEZI ,MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA WATOTO WENYE ULEMAVU



5:13 AM (1 hour ago)
Bweni lililojengwa kwaajili ya wanafunzi wenye uhitaji maalum shule ya msingi Ipyana .
Na Baraka Messa, Songwe
KUNDI la watoto wenye ulemavu limekuwa ni waathirika zaidi pale mazingira ya kujifunzia yanapokuwa siyo rafiki kwa mtoto mwenye umri chini ya miaka 8.Kundi hili linaweza kupata
athari mara mbizi zaidi ya mtoto asiye na ulemavu.

Mazingira mengi ya kujifunza yamelengwa kukidhi mahitaji ya watoto wasio na ulemavu,kuanzia madarasa,mazingira ya shule,vyoo na hata viwanja vya michezo,kitu ambacho
ni kinyume na miongozo na sera ya elimu nchini inayohimiza mazingira rafiki ya kujifunzia kwa
watoto wenye ulemavu.

Shule ni hatua muhimu kwa watoto kwenye makuzi,malezi na maendeleo ya awali ili kuijenga
kesho iliyo bora ya mtoto kabla ya kuvuka miaka nane.

Hii ni hatua ambayo ubongo wa mtoto unaanza kujengewa uwezo kwenye ujuzi,maarifa,ufahamu na hata namna ya kukabiliana na mazingira yanayozumzukunga katika siku za usoni za ukuaji wake.

Ili kumfanya mtoto aweze kupata malezi,makuzi na maendeleo bora ya awali,program jumuishi ya taifa ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali nchini inahimiza juu ya mazingira
rafiki,shawishi na jengefu kwa mtoto hususani ubongo na  saikolojia ya mtoto kwa watoto wote wasio na ulemavu na wenye ulemavu.

Katika Wilaya ya Ileje mkoani Songwe kumekuwa nachangamoto ya Malezi na Makuzi kwa watoto wenye ulemavu hasa kunyimwa haki yao ya Msingi ya kupata elimu kuanzia elimu ya awali  na Msingi kwa kisingizio cha ulemavu . 
Kutokana na changamoto za watoto wenye mahitaji Maalum 
kutopewa kipaumbele katika suala muhimu la elimu, wilaya ya Ileje imeanza kuimalisha miundo mbinu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa  bweni litakalo kuwa na uwezo wa kuchukua watoto wenye uhitaji Maalum 300 katika shule
ya Msingi Ipapa.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Farida Mgomi amesema kumekuwa na changamoto nyingi kwa watoto wenye uhitaji Maalum ikiwa ni pamoja na kunyimwa haki yao muhimu ya kupelekwa shule.

Anasema jambo hilo limewasukuma Wilaya hiyo kuanzisha ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule ya msingi Ipapa iliyopo Kata ya Isongole Wilaya hapo
ambapo  mpaka kukamilika litagharimu Sh 100 milioni.

"Kukamilika kwa bweni hilo kutatua changamoto za watoto wengi wenye mahitaji maalum kuanzia elimu ya awali na Msingi kupata haki yao ya Msingi ya kupata elimu, hasa wale
wanaofichwa majumbani" amesema.

Wataalam wa masualam ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto chini ya miaka nane wanasema mazingira yasipokuwa rafiki mbali na kuathiri ukuaji wa ubongo wa mtoto lakini pia yanachochea utoro na hata wengine kukatisha   masomo  hususani kwa watoto wenye ulemavu
ambao wanahitaji amzingira rafiki zaidi.

Ileje yenye wanafunzi 300 wenye ulemavu imeanza kutekekeleza mradi wa ujenzi wa bweni  ilikuweka mazingira rafiki kwa watoto wenye uemavu huku hali ya kustua ikiwa ni kasi ndogo ya ujenzi wa bweni hilo ambalo Machi 22,2024.

 Wakati wa ukaguzi wa maendeleo yake  ilionesha hali ya kusua sua kwa ujenzi wa  bweni hilo  licha ya kuwepo kwa vifaa kama  rangi,saruji hali imebainika  ni usimamizi mbovu wa miradi ya maendeleo.

Awali serikali ilitoa fedha Sh, 100 millioni kwa ajili ya kukamilisha mradi huo ili kupunguza adha kwa wanafunzi 300 wenye ulemavu kupata elimu bora na kuondoa changamoto
zinazowakabili.

Kwa mujibu wa mkuu wa Wilaya ya Ileje, Bi Farida Mgomi, Serikali baada ya kuleta milioni 100 za awali imeongeza tena shilingi milioni, 158 kwa ajili ya  ujenzi wa  bweni na uzio kwa
lengo la kuweka mazingira rafiki na shawishi ya kusomea pamoja na kuhakikisha ulinzi na usalama wa watoto hususani wale wenye ulemavu
 
Kwa upande wake Mwita Isaya kutoka Asas isiyo ya kiserikali ya HIMSO ambayo ni kinara katika masuala ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali katika mkoa wa Songwe amesema
Wilaya ya Ileje na mkoa wa Songwe kwa ujumla kumekuwa na changamoto ya Malezi yanayopeleke mtoto kutofikia ukuaji sahihi.

"Katika mkoa wetu wa Songwe kati ya watoto 100 ni watoto 24 ndio wanapitia malezi sahihi yenye mwitikio, wazazi na Jamii ya mkoa wa Songwe inatakiwa kubadilika katika masuala
muhimu ya kulea watoto na kuhakikisha wanapata elimu muhimu kuanzia elimu ya awali"  amesema Chacha.

Akiongelea kuhusu wa wazazi ambao wamekuwa na tabia ya kuwaficha watoto walemavu amewataka kuacha na badala yake wawape nafas ya kupelekwa shule kupata elimu kuanzia
elimu ya awali ili wawe na uwezo wa kujitegemea kwa baadae.

Mwananchi Samsoni Mshani amesema kukamilika kwa bweni hilo la watoto wenye mahitaji Maalum kutasaidia na  kuhamasisha wananchi wengi kupeleka watoto walemavu kupata masomo, kwa sababu wengine huogopa kuwapeleka shule kwa sababu ya watoto  wengi kuhitajiukaribu wa kuwasindikiza kila siku , jambo ambalo huona kama shughuli zao  husimama.

"Kukiwa na bweni wengi wataleta watoto kwa sababu , wazazi au walezi hawatapata usumbufu wa kuwapeleka na kuwafuata watoto asubuhi na muda wa kurud shule" amesema Mshani.

Mwongozo wa Serikali wa mwaka 2016 wa elimu bila malipo hujumuisha elimu ya awali kwa watoto wote waliofikia umri sahihi kuanza masomo bila kubagua walemavu.







Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464