JESHI LA POLISI SHINYANGA LAKAMATA VIFAA MBALIMBALI YAKIWEMO MAFUTA YA DIZELI LITA 320, VIPANDE 250 VYA NONDO NA NYAYA ZA UMEME

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kennedy Mgani akionyesha mitambo ya kutengenezea gongo

Na Suzy Butondo Shinyanga press blog

Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limekamata vitu mbalimbali yakiwemo mafuta ya dizeli lita 320, vipande 250 vya nondo, nyaya mbalimbali za umeme, matairi matano ya gari, injini moja ya pikipiki, betri sita za gari na mashine moja ya kukatia miti (chain saw).

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kennedy Mgani akitoa taarifa leo 17,4,2024 kwa waandishi wa habari amesema vifaa hivyo vimekamatwa wakati jeshi hilo likifanya misako pamoja na operesheni mbalimbali katika kipindi cha wiki tatu kuanzia Machi 28,2024 mpaka Aprili 16,2024.

Mgani amevitaja vifaa vingine vilivyoibiwa kuwa ni mitambo minne ya kutengeneza pombe ya moshi (Gongo) pombe ya moshi lita 13, bhangi kete 33, simu tano, pikipiki nne, mashine moja ya bonanza, Redio mbili, mtungi moja wa gas,Tv moja pamoja na vifaa mbalimbali vya kupigia ramli chonganishi.

"Jumla ya kesi tisa zimepata mafanikio ambapo kesi moja ya kubaka, ambapo mshitakiwa alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, kesi mbili kwa kupatikana bhangi washitakiwa wawili walihukumiwa kifungo cha miaka miwili mpaka mitatu jela, kesi moja kuvunja nyumba usiku na kuiba mshitakiwa mmoja alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela"ameeleza Mgani.

Amesema kesi moja kuharibu mali mshitakiwa alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela, kesi tatu za wizi washtakiwa watatu walihukumiwa kifungo cha miezi sita jela na kesi moja kuingia kwa jinai mshitakiwa alihukumiwa kifungo cha miezi minne jela.

Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga kikosi cha Usalama barabarani limefanikiwa kukamata jumla ya makosa 3,771 ambapo makosa ya magari ni 2,836 na makosa ya bajaji na pikipiki ni 935 wahusika waliwajibishwa kwa kulipa faini za papo kwa papo.

Aidha jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga inawashukuru wananchi kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha usalama wa mkoa wa Shinyanga unakuwa shwari, pia linatoa wito kwa wananchi woteckuendelea kutii na kufuata sheria na halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayekiuka sheria za nchi.




Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kennedy Mganiakionyesha nondo na nyaya za umeme zilizokamatwa

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kennedy Mgani akionyesha mitambo ya kutengenezea gongo

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kennedy Mgani akionyesha Simu zilizokamatwa
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kennedy Mgani akizungumza
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kennedy Mgani akionyesha pikipiki zilizokamatwa
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kennedy Mgani akionyesha madumu ya mafuta ya dizeli yaliyokamatwa




Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464