Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi akizungumza kwenye kikao cha baraza la Jumuiya ya Wazazi mkoa
Na Suzy Butondo Shinyanga blog
Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga imetambulisha rasmi kamati ndogo ya maadili na kamati ya uchumi miradi na fedha, ambazo zitasimamia miradi mbalimbali ya jumuiya ya wazazi mkoa wa Shinyanga, ambapo katika kamati hizo wapo wabunge wa majimbo yote ya mkoa wa Shinyanga.
Kamati hizo zimetambulishwa leo 27,4,2024 kwenye kikao cha baraza la wazazi mkoa kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa CCM Mkoani hapa, huku kamati ya uchumi miradi na fedha ikiwa na wajumbe 20, na kamati ya maadili watu 10 .
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi John Siagi aliwataja wajumbe wa kamati ya uchumi miradi na fedha kuwa ni Isack Nganga, Nael Msomi,Joseph Mshandete,Adonkam Kweka,Suzy Luhende, Bahati Dede,Matemla,Leonard Jambo,Flano Masanja, ,Halidy Rajabu,Daniel Mapunda,Andrew Ntinginya,Mwita Little tresure,
Wengine ni Joseph Kahama,Joseph Elias Luhanga Jumanne wagana,mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani,mbunge wa jimbo la Msalala Iddy Kassim Iddy, na Patrobas Katambi.
Pia mwenyekiti Siagi amewataja wajumbe wa kamati ya maadili kuwa ni Alhaji Salm Simba,Ziporah Pangani,James Kusekwa,Jobu Nganyange,diwani viti maalumu Ester Makune,Mbunge wa jimbo la Kahama Jumanne Kishimba, mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo,Perpetua Masesa,Mary Izengo na Amir Husein
Siagi amezishauri kamati hizo zifanye kazi kwa kushirikiana na jumuiya ya wazazi Mkoa ili kuhakikisha Jumuiya hiyo inapata maendeleo makubwa na chama chake.
"Niwaombe tu wote mlioteuliwa kuanzia leo muanze kufanya kazi ili kuhakikisha chama na jumuiya hii inakuwa imara na kusimamia miradi mbalimbali ili kuhakikisha inakuwa imara haichakachuliwi, naamini wote mko imara hakuna cha kuwakwamisha" alisema Siagi.
Pia aliwaomba makatibu na wenyeviti wa wilaya waongeze jitihada za kuhakikisha mikutano ya kata inafanyika kwa wakati, ikiwemo kusimamia kikamilifu suala la uchaguzi wa serikali za mitaa, ili kuhakikisha wanapatikana viongozi wenye sifa zinazotakiwa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.
"Kuna watu wanadhoofisha viongozi walioko madarakani na kutengeneza makundi ambayo sio mazuri, hivyo tunatakiwa tuyakemee hayo, ili kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo kikubwa,tuwaombe sana mnaporudi mawilayani mhakikishe mnapata watu wazuri wa kuweza kukivusha chama ili nafasi zetu zote ziweze kurudi, pia tukemee mabaya yanayoendelea kule kwenye maeneo yetu"amesema Siagi.
Katibu wa Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu amesema anawashukuru wajumbe wote walioteuliwa kwa kukubali, kwani wamefanya uteuzi huo kwa kufuata kanuni inavyoelekeza, hivyo anaamini watashirikiana na kamati zote ili kuhakikisha kila sekta inafanya vizuri na kuhakikisha uhai wa chama na jumuiya zake unaenda vizuri.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Msalala Iddy Kassim Iddy ambaye alihudhulia kwenye kikao hicho akizungumza kwa niaba ya wabunge wote aliushukuru uongozi kwa kuwateuwa wabunge wa majimbo ambapo ameahidi kwamba watatoa ushirikiano mzuri katika kuijenga jumuiya ya wazazi na CCM.
Aidha mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Mkoa Siagi katika kikao hicho aliwakabidhi wabunge wa majimbo ya Mkoa wa Shinyanga vyeti vya pongezi kwa kutoa ushirikiano mbalimbali katika Jumuiya hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi akizungumza kwenye kikao cha baraza la Jumuiya hiyo
Mbunge wa jimbo la Msalala Iddy Kassim Iddy akikabidhiwa cheti cha pongezi na mwenyekiti wa wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi
Katibu wa mbunge wa jimbo la Kishapu Ndilla Nchimika akikabidhiwa cheti cha pongezi na mwenyekiti wa wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi
Mjumbe wa kamati ya fedha miradi na uchumi akijitambulisha
Wajumbe wa baraza wakiwa kwenye kikao