MKOA WA GEITA WAKWAMA UANDIKISHAJI WANAFUNZI WA DARASA LA AWALI

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la awali.

Salum Maige, Geita

 Mkoa wa Geita umekwama kufikia lengo la kuandikisha wanafunzi wa darasa la awali  kwa mwaka wa masomo wa 2024 kutoka lengo la kuandikisha wanafunzila 108,385 mpaka 84,609 wavulana wakiwa ni 41,983 na waschana 42,625 sawa na asilimia 78 mpaka zoezi lilipokuwa linakamilika machi 31,mwaka huu.

 Kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana,  idadi hiyo imeongezeka kutoka wanafunzi 75,053 wavulana 36,907 na waschana 38,146 sawa na asilimia 113.36  walioandikishwakwamwakawa masomo wa 2023 baada ya kuvuka lengo lililokuwa limewekwa na mkoa huo la kuandikisha wanafunzi 66,362.

 Kwa upande wa darasa la kwanza kwanza malengo yalikuwa ni kuandikisha wanafunzi 98,362 na kwamba mkoa umevuka malengo baada ya kufanikiwa kuandikisha wanafunzi 112,220 wavulana 55,762 nawasichana 56,458 sawanaasilimia 114.

 Kwa mujibu wa afisa elimu mkoa wa Geita Antony Mtweve ni kwamba idadi hiyo imepungua ukilinganisha wanafunzi 112,913 wavulana 56,700 na waschana 56,213 walioandikishwa kuanza darasa la kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2023 sawa na asilimia 110.39.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kharumwa wilaya ya Nyang’hwale mkoani humo walisema, kikwazo cha kutofikia malengo inawezakuwa umbali wa kwenda shule ukilinganisha na umri wa mtoto anayetakiwa kuanza darasa la awali.

 Husein Ally mkazi wa kijiji hicho anasema, ipo haja ya serikali kushirikiana na wananchi kuanzisha shule shikizi za wanafunzi wa madarasa ya awali ili kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shule.

 “Shule shikizi zikianzishwa katika maeneo ya vitongoji na mitaa iliyo mbali na shule inaweza kusaidia hawa watoto kusoma karibu na maeneo yao ya nyumbani ,sikwamba wazazi hatupendi mtoto kusoma darasa la awali isipokuwa umbali”, anasema Ally.

 Annastazia James ambaye ni mkazi wa mtaa wa Nyakabale anazitaja sababu zingine zinazochangia kuwa ni hali ngumu ya maisha kwa baadhi ya wazazi kushindwa kununua mahitaji ya shule kama vile madaftari na sare.

 Hata hivyo, baadhiya  wazazi wamekiri kwamba uhamasishaji wa kuandikisha watoto ulikuwa ni mkubwa kupitia mikutano ya hadhara ambapo walitangaziwa na viongozi kwenda kuandikisha watoto wao.

 “Labda mzazi anayeshindwa kuandikisha mtoto wake atakuwa na matatizo yake binafsi labda hali ngumu ya maisha,kwanza mtoto unaacha kumpeleka shule iliiweje,mtoto mdogo hata akibaki nyumbani atakusaidia nini wewe kama mzazi?”,  alihoji Salome Cherehani.

 Afisa elimu taaluma mkoa wa Geita Cassian Luoga amekiri kuwa sababu zilizotajwa na baadhi ya wazazi ni moja changamoto zilizobainishwa na mkoa zikiwemo za umri mdogo wa watoto ukilinganisha na umbali wa kutoka nyumbani kwenda shuleni.

 Sababu nyingine ni mvua zinazoendelea kunyesha wakihofia watoto kusombwa na maji wakati wa kutoka na kwenda shuleni.

 “Umbali kutoka kwenye majumba yao kwenda shule zilizopo inakuwa ni ngumu sana ukilinganisha na umri wao,lakini tunawapa elimu wazazi walau kuwasindikiza watoto kwenda na kutoka shule na kuwafuata ili tu wapate haki yao ya elimu ya awali ambayo ndiyo msingi wa elimu”, anasema Luoga.

 Kwa upande wake afisa elimu Mtweve ametaja sababu zingine zazilizosababisha kukwama kufikia lengo ni mwamko mdogo wa wazazi kuandikisha watoto wao kuanza darasa la awali na badala yake baadhi yao husubiri kuandikisha darasa la kwanza.

 “Nilichokibaini kwa wanafunzi wa awali wazazi hawaoni kama elimu inaanzia darasa la awali na sio darasa la kwanza ,hivyo wazazi hawajitokezi sana wakiwa hawaamini kwamba mfumo wa elimu unaanzia darasa la awali”, anasemaMtweve.

 Ameongeza kuwa mkoa wa Geita una jumla ya madarasa 15 yanayozungumza yaliyojengwa na serikali kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la awali ambayo yamejengwa katika kila halmashauri na idara ya elimu imewaelekeza walimu kutengeneza zana za kujifunzia watoto.

  “Mtoto akikosa elimu ya awali mwendelezo wa mfumo wa elimu ya awali anakuwa hana ,hivyo inampa wakati mgumu mwalimu anapokuwa anafundisha ambapo ambaye hakupita darasa la awali uelewa wake unakuwa tofauti yule aliyepita darasa la awali.

 Uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali ni utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo nchini Tanzania ya mwaka 2014  inayojumuisha elimu ya awali katika elimu ya msingi kwa kuzitaka shule zote za msingi kuwa nadarasa la elimu ya awali kwa mtoto chini ya miaka mitano.

 Katika taarifaya program jumuishi ya taifa ya malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto(PJT-MMMAM) iliyozinduliwa disemba 2021 inaonyesha kuwa sera hiyo imechochea ongezeko la uandikishaji wa watoto katika elimu ya awali kufikia 500,000 ndani ya mwaka mmoja kutoka 1,069,823 mwaka 2015 mpaka 1,562770 mwaka 2016.

 





 

 

 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464