Na stella Homolwa,Shinyanga Press Club Blog
Shirika la Compassion
International Tanzania Klasta ya Igunga limeadhimisha miaka 25 ya Shirika
hilo,kwa kutoa msaada kwa makundi mbalimbali,vikiwemo vitabu na vifaa vya
michezo kwa shule za Msingi.
Mkurugenzi wa Vituo vya
huduma ya mtoto Klasta ya Igunga Manase Silasi amesema katika maadhimisho hayo pia
wameshiriki katika usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada
za serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Amesema Shirika la Compassion International kwa Wilaya ya
Igunga linahudumia watoto zaidi ya 800 kupitia kwenye Vituo vyake ambapo
wanawawezesha kuwajenga kiimani na kuwapatia huduma zote muhimu ikiwemo
elimu,matibabu na kuhakikisha wanakaa kwenye mazingira mazuri.
Amesema wamegawa Vitabu na vifaa vya michezo
katika shule mbalimbali za Wilaya ya Igunga ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha
miaka 25 ya Compasion katika vituo vya
huduma na maendeleo ya mtoto na kijana
Klasta ya Igunga Mkoani Tabora.
Mkurugenzi wa vituo vya
huduma ya mtoto klasta ya Igunga Manase Silasi amesema wameamuwa kuadhimisha
miaka 25 ya shirika la Compassion kwa kuwafikia wanafunzi pamoja na kusisitiza
umuhimu wa kutunza mazingira na kusaidia makundi ya watu wenye mahitaji maalumu
katika jamii.
Wakizungumza baada ya kukabidhi vitabu na vifaa vya michezo baadhi ya viongozi wa dini na walimu wamesema kuna umuhimu wa kuwekeza katika elimu na kusisitiza suala la maadili kwa vijana kutokana na kuwa na utandawazi na watu kufanya vitendo vya ukatili.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464