WANANCHI 23,361 WA KATA MWALUGULU KUNUFAIKA NA FEDHA ZA TOZO NA MIAMALA YA SIMU KWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Mboni Mhita akiongoza watumishi wa serikali kukagua maendeleo ya kituo cha afya kata ya Mwalugulu
Na sebastian Mnakaya-Kahama
Serikali ya imeipatia halmashauri ya msalala wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kiasi cha shilingi milioni 500 kupita fedha za tozo na mihamala kwa ajili ya kutekelezaji mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha mwalugulu ambacho kikikamilika kitaweza hudumia wananchi 23,631.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa kituo hicho mbele ya mkuu wa wilaya ya Kahama MBONI MHITA, kaimu mganga mfawidhi wa kituo hicho ESTER MWATWINA, amesema fedha hizo hazikutosha kukamilisha ujenzi huo na halamshauri ya msalala kupitia mapato ya ndani iliongeza kiasi cha shingili milioni 40 ili kukamilisha majengo hayo.
"Kituo hichi cha afya kikikamilia na kuanza kazi kitaweza kuhudumia wananchi ya 23,631 na kutakuwa na zahanati nne ambazo zitategemea kituo hicho cha afya Mwalugulu ambazo ni Sungamile, mwakima, Bane na Kilimbo," Dr Ester
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama MBONI MHITA amesema kuwa fedha zilizokuwa zinalalamikiwa baadhi ya wananchi nchini za tozo simu na mihamala leo zinatekeleza mradi miradi mbalimbali ya maendeleo na kukamilisha, mojawapo ikiwa ni kituo cha afya mwalugulu.
" hii milion 500 ambayo imetolewa na serikali kuu haikutoka kwenye bajeti nyingine bali imetoka kwenye bajeti ya tozo za simu, ambazo kipindi inapelekwa bungeni kama mswada watu walipiga kelele sana ila leo zimeleta matunda kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama jinsi kituo hichi kinavyojengwa,"amesema Mboni Mhita.
Nae, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya msalala HAMISI KATIMBA amesema kuwa wataendelea kutoa fedha za mapato ya ndani ili kuweza kukamilisha miradi mbalimbali, huku halmashauri hiyo ikiendelea kukusanya mapato kwa vyanzo mbalimbali kwa wingi.
"Gharama halisi ya kumalizia miundombinu hiyo ambayo inatakiwa ijengwe ilikuwa shilingi milion 80 kwa hiyo kwa kuanzia tulitoa shilingi milioni 40 na pia iliyobakia tutamalizia kwa kupitia mapato ya ndani kwa kuleta fedha kwa haraka ili kukamilisha ili kituo kianze kufanyakazi," amesema Hamis Katimba.
Mhandisi,Juma magoto wa Halmashauri ya Msalala akitoa maelezo juu ya ujenzi uanavyoendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464