SERIKALI IMEJENGA SHULE 26 ZA WASICHANA ZA BWENI ZINAZOFUNDISHA SAYANSI

Katika kuimarisha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika shule za msingi na sekondari, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanikiwa kuwezesha ujenzi wa shule mpya za sekondari ngazi ya kata 228 na 26 za Sayansi za wasichana za bweni za mikoa. 

Hayo yamebainishwa leo Jumanne Mei 07, 2024 na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda alipokuwa akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2024/25 ambapo amesema kuwa Serikali pia mewezesha ujenzi wa shule mpya za msingi 302 nchi nzima.

"Serikali imewezesha ujenzi wa madarasa 4,140, maabara 18, mabweni 119, matundu ya vyoo 21,237 na nyumba za walimu 285 zenye uwezo wa kuchukua watumishi 456 katika shule za msingi na sekondari, pi imewezesha ukamilishaji wa ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa 869, maabara za sayansi 132 na matundu ya vyoo 1,650 katika shule mbalimbali nchini", amesema.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464