Mkurugenzi wa Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume, akifungua mkutano wakati wa Utambulisho wa Mradi wa Huduma na Matibabu ya VVU (Afya Thabiti) unaofadhiliwa na PEPFAR kupitia CDC Tanzania na kutekelezwa na Amref Tanzania kwa kushirikiana na CIHEB Tanzania, TCDC Tanzania, na Afya plus timu za afya za mikoa na halmashauri (R/CHMT) katika mikoa ya Simiyu, Mara na visiwani Zanzibar. Katika Ukumbi wa Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dodoma 20-5 2024.
Mkurugenzi wa Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume, akifungua mkutano wakati wa Utambulisho wa Mradi wa Huduma na Matibabu ya VVU (Afya Thabiti) unaofadhiliwa na PEPFAR kupitia CDC Tanzania na kutekelezwa na Amref Tanzania kwa kushirikiana na CIHEB Tanzania, TCDC Tanzania, na Afya plus timu za afya za mikoa na halmashauri (R/CHMT) katika mikoa ya Simiyu, Mara na visiwani Zanzibar. Katika Ukumbi wa Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dodoma 20-5 2024.
Mkurugenzi wa Mradi wa Afya Thabiti Amref Tanzania, Dkt. Edwin Kilimba akizungumza wakati wa mkutano wa Utambulisho wa Mradi wa Huduma na Matibabu ya VVU (Afya Thabiti) TAMISEMI- kitengo cha Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe, katika Ukumbi wa Mkurugenzi wa Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dodoma 20-5 2024.
****
Amref Health Africa, Tanzania leo imefanya mkutano na Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, kwa lengo la kutambulisha Mradi wa Huduma na Matibabu ya VVU unaojulikana kama Afya Thabiti. Mradi huo unaofadhiliwa na PEPFAR kupitia CDC Tanzania na kutekelezwa na Amref Tanzania kwa kushirikiana na CIHEB Tanzania, TCDC Tanzania, na Afya plus unalenga kuimarisha utoaji wa huduma na matibabu ya kufubaza VVU katika Kliniki za VVU/UKIMWI za serikali na za hospitali teule ili kuongeza kasi ya kufikia malengo ya 95-95-95 ya kudhibiti janga la UKIMWI nchini.
Mkutano huo uliohudhuriwa na wafanyakazi mbalimbali kutoka TAMISEMI idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt. Rashid Mfaume, ambaye alisema "Serikali kupitia TAMISEMI kwa ujumla imeendelea kufanya kazi na wadau katika kutekeleza afua mbalimbali za kiafya, kuboresha miundombinu na kutoa huduma za afya kwa walengwa. Serikali imejipanga kuhakikisha inafikia lengo la dunia la kutokomeza janga la UKIMWI ifikapo 2030.
Akizungumza na washiriki, Dkt. Rashid Mfaume alisema “Leo hii katika kuendeleza wajibu wake na kuunga mkono jitihada za serikali, Shirika linatekeleza mradi wa Afya Thabiti kuanzia October 2023 mpaka Septemba 2028 katika mikoa ya Mara, Simiyu pamoja na Zanzibar. Matarajio ya serikali ni mradi kuendeleza mafanikio ya miaka 5 iliyopita na kuendelea kupunguza au kumaliza maambukizi mapya kwenye maeneo ya mradi.
Kwa upande wake, Daktari Edwin Kilimba, Mkurugenzi wa Mradi wa Afya Thabiti, akimwakilisha Daktari Florence Temu, Mkurugenzi Mkaazi wa Amref Tanzania, alisema "Tunaamini ushirikiano wa karibu na wenzetu katika mikoa ya Mara na Simiyu utatusaidia kufanikisha lengo la serikali katika kutoa huduma za afya kwa wananchi wote."
Amref Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wizara zote, mashirika ya serikali, wafadhili, mashirika ya kijamii (CBOs), mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), sekta binafsi, na wanajamii katika kuchangia upatikanaji sawa na endelevu wa huduma bora za afya ya msingi (PHC) na hatimaye kuchangia katika kufanikisha huduma ya afya kwa wote (UHC) nchini Tanzania.