EWURA WATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA,KUANDIKA HABARI KWA USAHIHI ZA NISHATI NA MAJI
MAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi, wametoa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Shinyanga, juu ya kufahamu majukumu yake na kutoa habari zenye usahihi kwa wananchi,wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kutafuta habari.
Mafunzo hayo yameanza kutolewa leo Mei 2,2024 ambayo yatachukua muda wa siku mbili, ambapo kesho waandishi wa habari watatembelea chanzo cha Maji ya Ziwa Victoria kilichopo Ihelele wilayani Misungwi mkoani Mwanza, chanzo ambacho kinazalisha Maji na kupeleka mkoani Shinyanga na Mikoa mingine.
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Walter Christopher, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina hiyo, amesema waandishi wa habari wakielimika vizuri na kufahamu majukumu ya Ewura, wataandika habari zao kwa usahihi na kuhabarisha umma.
“Tukielimisha waandishi wa habari,tumeielimisha jamii”amesema Christopher.
Aidha, amewapongeza waandishi wa habari mkoani humo, kwa kuandika andiko la maombi ya kupata mafunzo hayo, ambayo pia watakuwa wakiyatoa kwa waandishi wa habari katika Mikoa migine ili kupata ulewa zaidi juu ya majukumu ya EWURA.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC)Patrick Mabula,akizungumza kwenye Semina hiyo ameishukuru EWURA kwa kukubali maombi ya Klabu hiyo na kutoa mafunzo hayo, ambayo yatawaongezea uelewa katika utekelezaji wa majukumu yao.
Amesema jamii inawatengemea waandishi wa habari, katika kuwahabarisha habari mbalimbali sababu ndiyo kioo chao, hivyo kufahamu majukumu ya EWURA,watakuwa wakiandika habari zao kwa usahihi za huduma ya Nishati na Maji.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Walter Christopher,akizungumza kwenye mafunzo ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga,
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Walter Christopher,akizungumza kwenye mafunzo ya waandishi wa habari Mkoani Shinyanga.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC)Patrick Mabula akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Mwandamizi Idara ya Mafuta kutoka EWURA Mhandisi Ibrahimu Kajugusi akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mjumbe wa EWURA CCC Mkoa wa Shinyanga Joseph Ndatala akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Mwandamizi Uhusiano kwa Umma kutoka EWURA Tobietha Makafu akielezea Majukumu ya EWURA.
Afisa Mwandamizi Uhusiano kwa Umma kutoka EWURA Tobietha Wakafu akielezea Majukumu ya EWURA.
Afisa Mwandamizi Huduma kwa Wateja kutoka EWURA Kanda ya Magharibi Getruda Mbilingi akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Afisa Mwandamizi Huduma kwa Wateja kutoka EWURA Kanda ya Magharibi Getruda Mbilingi akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo ya EWURA.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya EWURA.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya EWURA.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya EWURA.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya EWURA.
Waandishi wa habari wakiendelea na mafunzo ya EWURA.
Mafunzo ya EWURA yakiendelea.
Mafunzo ya EWURA yakiendelea.
Mafunzo ya EWURA yakiendelea.
Mafunzo ya EWURA yakiendelea.
Picha ya pamoja ikipigwa kwenye mafunzo ya EWURA.
Picha ya pamoja ikipigwa kwenye mafunzo ya EWURA.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464