MWENYEKITI WA HALMASHAURI SHYDC NGASSA MBOJE AMEWAAGIZA WATENDAJI WA VIJIJI KUWASOMEA WANANCHI MAPATO NA MATUMIZI


Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, amewaagiza Watendaji wa Vijiji wilayani humo, wawe wanawasomea wananchi Mapato na Matumizi.

Ametoa maagizo hayo leo Mei 8,2024 kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wilayani humo ambalo lilikuwa na Ajenda mbalimbali ikiwamo ya uwasilishaji wa Taarifa za Kata.
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Shinyanga Stewart Makali.

Amesema katika Kikao hicho cha Baraza kuna Masuala ambayo ameyagundua yaliyoibua Mijadala,ikiwamo Watendaji wa Vijiji kutosomea wananchi mapato na matumizi.
"Watendaji wa Vijiji ambao ndiyo Makatibu,wasomeeni Mapato na Matumizi wananchi wenu, ili kutoleta Migogoro na Sintofahamu kuwa huenda pesa zao zimeliwa,"amesema Mboje.

Aidha,ameagiza pia kuwepo na Mawasiliano mazuri ya taarifa kati ya Watendaji wa Kata na Madiwani ambayo ndiyo Wenyeviti wa Kamati ya Kata (WARDS)ili kusiwepo na mkanganyiko.
Katika baraza hilo kila diwani amewasilisha taarifa zake za Kata.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464