WEADO WAMEFANYA MAJADILIANO NA MABARAZA YA WATOTO,WALIMU WALEZI JUU ULINZI WA HAKI ZA MTOTO NA STADI ZA MAISHA LYABUKANDE WILAYANI SHINYANGA
SHIRIKA la WEADO limefanya majadiliano na Mabaraza ya watoto na walimu walezi kwa shule za Msingi na Sekondari Kata ya Lyabukande wilayani Shinyanga juu ya ulinzi wa haki za Mtoto na Stadi za maisha.
Majadaliano hayo yamefanyika leo Mei 10,2024 katika shule ya Msingi Lyabukande ambayo yalihudhuliwa pia na viongozi ngazi ya Kata akiwamo Afisa Maendeleo ya Jamii,Mtendaji wa Kata na Afisa Elimu,ambapo Shirika la WEADO linatekeleza wa chukua hatua sasa zuia ukatili kwenye Kata hiyo kwa ufadhili wa WFT-Trust.
Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko akizungumza kwenye kikao hicho,amesema wanajadili viashiria hatarishi vinavyosababisha ukatili dhidi ya watoto,ili kuifanya Lyabukande kuwa na Jamii inayozingatia usawa na haki za watoto.
"Mradi wetu huu ni kuzuia ukatili dhidi ya watoto kwa kuhakikisha ulinzi na usalama kwa watoto unaimarishwa, pamoja na kuvishughulikia viashiria vinavyosababisha ukatili kwa mtoto," amesema Nnko.
Aidha,amewataka pia Walimu walezi kuwa walinzi wa Watoto kwa kuhakikisha usalama wao pamoja na Malezi bora.
Mratibu wa mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatii dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) wilayani Shinyanga Aisha Omary amewataka Walimu walezi kuhuisha Mabaraza ya Watoto pamoja na kuweka Masanduka ya Maoni Shuleni, ili kusaidia kupata taarifa za ukatili na kuchukua hatua.
Afisa Elimu Kata ya Lyabukande Juma Chiaba naye amesisitiza Mabara hayo ya watoto yawe yanakaa vikao mara tatu kwa wiki kwa mujibu wa muongozo kwa kusimamiwa na Walimu walezi, hali ambayo itasaidia kusimamia haki za watoto.
Mtendaji wa Kata ya Lyabukande Shadrack Maduhu, amemuagiza Afisa Maendeleo wa Kata hiyo Salum Mwang'imba kwamba kuanzia siku ya jumatatu aanze kupita shuleni ili kuimarisha Mabaraza ya watoto kwa kushirikiana na Walimu Walezi.
Amesema changamoto zote ambazo zimeainishwa na Watoto kwenye Majadiliano ikiwamo ya kuvutishwa Bangi au Sigara kwenye vikundi vya Kilimo kwamba atafanya ufuatiliaji na kuchukua hatua.
Katika majadiliano hayo watoto wametaja baadhi ya maeneo hatarishi kwao ambayo ni chanzo cha kufanyiwa ukatili kuwa ni maeneo ya Minada, Magurio,Machungaji,Kisenya kuni, Sentani,Saloon, Vibanda Umiza na kwenye Vikundi vya Kilimo ambavyo hufanya vibarua.
Aidha,mbali na Majadiliano hayo pia kwenye kikao hicho yametolewa mafunzo kwa Walimu Walezi juu ya utambuzi wa Mtoto aliyefanyiwa ukatili, pamoja na ukatili dhidi ya watoto Mtandaoni.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko akizungumza na Walimu Walezi wa Mabaraza ya Watoto Lyabukande.
Mratibu wa MTAKUWWA Wilayani Shinyanga Aisha Omary akizungumza kwenye kikao hicho.
Mratibu wa MTAKUWWA Wilayani Shinyanga Aisha Omary akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Elimu Kata ya Lyabukande Juma Chiaba akizungumza kwenye kikao hicho.
Mtendaji wa Kata ya Lyabukande Shadrack Maduhu akizungumza kwenye kikao hicho.
Mratibu wa Mradi wa chukua hatua sasa,zuia ukatili kutoka Shirika la WEADO John Eddy akizungumza na Walimu Walezi wa Mabaraza ya Watoto Lyabukande.
Afisa ufuatiliaji na Tathimini wa Mradi kutoka Shirika la WEADO Kadeth Geogre akizungumza na Mabaraza ya Watoto Lyabukande.
Kikao cha Majadiliano kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha ya pamoja ikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464