Rais wa Iran afariki kwa ajali ya Helikopta
Rais wa Iran Ebrahim Raisi pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Hossein Amir-Abdollahian na wengine kadhaa wamethibitishwa kufariki dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea jana Jumapili Kaskazini-Magharibi mwa Iran hii ni kwa mujibu wa runinga ya Taifa hilo.
Rais wa Iran Ebrahim Raisi
Taarifa za awali zilieleza kuwa hali mbaya ya hewa ikiwemo ukungu katika eneo ilipotokea ajali hiyo, ulifanya helikopta hiyo kushindwa kutua wakati Rais huyo na ujumbe wake wakielekea mji wa Tabriz uliopo Kaskazini Magharibi mwa Iran.
Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu mapema leo waokoaji walilipata eneo ilipoanguka helikopta hiyo na kuelezwa kwamba ulikuwa imeteketea kabisa.
Helikopta hiyo ni miongoni mwa helikopta tatu zilzokuwa katika msafara huo, ambapo mbili inaelezwa zilitua salama.
Chanzo:EATV