POLISI:JUMIKITA WEKENI UTARATIBU WA KUDHIBITI WALE WANAOHARIBU TASWIRA YA HABARI MITANDAONI

POLISI:JUMIKITA WEKENI UTARATIBU WA KUDHIBITI WALE WANAOHARIBU TASWIRA YA HABARI MITANDAONI

Na Marco Maduhu,Dar es salaam

MSEMAJI wa Jeshi la Polisi Nchini (SACP) David Msime,ameisisitiza Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA),kuweka utaratibu wa kudhibiti waandishi wa habari ambao wanaharibu taswira ya taaluma hiyo Mitandaoni.

Msime amebainisha hayo leo Mei 21,2024 kwenye Kongamano la Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) na Miaka ya Rais Samia Suluhu Hassani lililoendana sambamba na kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambayo kitaifa ilifanyika Mei 3 Jijini Dodoma.

Akizungumza wakati akiwasilisha Mada kwenye Kongamano hilo,juu ya Usalama na usimamizi kwenye Mitandao ya Kijamii, amesema ili kuwa salama na Matumizi ya Mitandao ya Kijamii, ni vyema waandishi wa habari wakazingatia Miiko,Maadili na Sheria za habari.

Amesema kuna baadhi ya waandishi wa habari wa Mitandaoni,wamekuwa hawazingatii Maadili wala Sheria za habari,wakilenga kutafuta wasomaji (Views) na hata kuharibu Taswira ya habari, na hivyo kuisihi JUMIKITA kuweka utaratibu wa kudhibiti waandishi wa namna hiyo.

"Kuna Masuala ya Muhimu ya Msisitizo JUMIKITA wekeni utaratibu wa kudhibiti wale wanaoharibu Taswira ya habari za Mitandaoni," amesema Msime.

Amewasihi pia waandishi wa habari za Mitandaoni, kuepuka kuandika habari zenye viashiria vya uchonganishi,kulinda Faragha za watu,kubalance habari,kuandika habari kwa kutanguliza uzalendo, na kuzingatia Amani,ulinzi na usalama wa Taifa.

Katika hatua nyingine amewataka waandishi wa habari,kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuepukana na utapeli wa mitandaoni, na kwamba uharifu sasa hivi umehamia Mitandaoni.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464