KATAMBI AKABIDHI MAGARI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SHINYANGA,AMPONGEZA RAIS SAMIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

KATAMBI AKABIDHI MAGARI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA SHINYANGA,AMPONGEZA RAIS SAMIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, amekanidhi Magari Matatu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga,huku akimpongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi na kuboresha huduma za Afya hapa nchini.

Magari yaliyokabidhiwa ni Gari Moja la kubeba Wagonjwa (Ambulance) Gari la Utawala la shughuli za usimamizi Shirikishi, pamoja na Gari aina ya TATA kwa ajili ya kubeba Watumishi wa Afya, na kuwapeleka kutoa huduma Hospitalini na kisha kuwarudisha majumbani mwao.
Amekabidhi Magari hayo leo Mei 24,2024 katika Viwanja vya Hospitalini hapo na kuhudhuliwa na Wananchi,viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama,pamoja na Madiwani.

Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye ulemavu, akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi Magari,amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwamba katika Utawala wake ndani ya kipindi kifupi, ameleta mageuzi makubwa katika Sekta ya Afya likiwamo Jimbo la Shinyanga Mjini.
“Leo ninakabidhi Magari haya Matatu katika Hospitali hii ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga ni jambo jema sana katika kuboresha huduma za Afya, na kuwajali Watumishi kwa kuwapatia Usafiri,tuna Mshukuru sana Rais Samia hapa Shinyanga katika ahadi zetu kweye Sekta ya Afya tumetekeleza zaidi ya asilimia 100 na kupitiliza kabisa, amesema Katambi.

Aidha, amesema kwa Changamoto ambazo zimetajwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ikiwamo na uchache wa Miundombinu ya Majengo, upungufu Watumishi, Ubovu wa Barabara kwamba atazifikisha sehemu husika ili zipate kutatuliwa, huku akibainisha kwamba kwa upande wa ujenzi wa Barabara Kiwango cha Lami lenye tayari lipo kwenye mchakato.

Katika hatua nyingine Katambi, amewapongeza Watumishi wa Afya kwa huduma nzuri ambayo wanaitoa kwa wananchi, na kuwasihi waendelee na Moyo huo huo,ili kuunga Juhudi za Rais Samia katika kuboresha huduma za matibabu kwa wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro, amesema mambo ambayo anayafanya Katambi Jimboni kwake ni Maajabu, na ni bahati ya pekee waliyonayo wanashinyanga, kuwa na Mbunge mpenda Maendeleo na hana Kelele, zaidi ya kuonyesha Vitendo.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko,amesisitiza kwamba Magari hayo yatumike kwa malengo kusudiwa pamoja na kutunzwa ile yadumu kwa muda mrefu kutoa huduma.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe, amemsihi Mbunge Katambi kwamba aendelee kuchapa kazi na kukaza uzi, katika kuwatumikia wananchi na kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dk. Luzila John, akisoma Risala amesema anampongeza Rais Samia namna alivyosaidia upatikanaji wa Magari hayo pamoja na Mbunge Katambi, sambamba na ufuatiliaji upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kukamilisha Miundombinu ya Majengo,kama vile Jengo la Mama na Mtoto, Mochwari, Jengo la kichomea Taka, Ufuaji na Maabara.

Ametaja Changamoto ambazo bado zinaikabili Hospitali hiyo kwamba ni Uchache wa Miundombinu ya Majengo, kwamba walipaswa kuna na Majengo 25 ili kukidhi utoaji wa huduma, lakini mpaka sasa wana Majengo Matano tu na kufanya kuwa na upungufu wa Majengo 20.
Changamoto zingine ni Upungufu wa Watumishi 225 sawa na asilimia 47, pamoja na ubovu wa Barabara ya kutoka Ndala kwenda Hospitalini hapo, na hivyo kuleta usumbufu wa Wagonjwa hasa walio Mahututi na kuvunjika Mifupa.
Picha za pamoja zikipigwa kwenye hafla hiyo ya kukabidhi Magari.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464