Jamii imeshauriwa kuwa mstari wa mbele kupinga ukatili wa kijinsia kwa Wanawake na Watoto kwa lengo la kuwa na jamii njema yenye kuwa na upendo na maadili.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa dawati la jinsia Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga SSP Monica Sehere wakati wa uoaji wa elimu ya kupinga ukatili chini ya mradi wa kujenga uelewa wa Sheria zinazomlinda Mtoto na Mwanamke katika jamii.
Akiongea na viongozi mbalimbali pamoja na wakazi wa kata ya Nyamalongo katika Halmashauri ya Shinyanga SSP Monica amesema vitendo vya ukatili vinapaswa kupigwa vita kwa nguzo zote kwa kushirikisha makundi mbalimbali.
Amewataka viongozi kuepuka tabia ya kusululisha kesi za ukatili badala yake kuzifikisha katika vyombo vya Sheria ili wahusika wachukuliwe hatua.
Kwa upande wao viongozi pamoja na wakazi wa kata hiyo wameahidi kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika kata hiyo .
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464