MISA-TAN WAMTUNUKU ZAWADI RAIS SAMIA KWA KUIMARISHA UHURU WA HABARI,KUJIELEZA NCHINI TANZANIA KATIKA KONGAMANO LA TAFAKURI YA MWAKA LA UHURU WA KUJIELEZA
Serikali inaendelea kufanya mapitio upya ya Sera ya habari 2003
TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN),wame Mtunuka zawadi ya picha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni pongezi kwa kuimarisha uhuru wa habari,kujieleza hapa nchini.
Zawadi hiyo imetolewa leo Mei 31,2024 kwenye Kongamano la Tafakuri ya Mwaka la Uhuru wa kujieleza lililoandaliwa na MISA-TAN Jijini Dar es Salaam kwa ufadhili wa Un Human Rights na Foundation For Civil Society, na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wa habari kutoka ndani ndani na Nje ya Nchi ambapo zawadi hiyo amekabidhiwa Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi kwa niaba ya Rais Samia, na Makamu Mwenyekiti wa MISA-TAN James Malenga.
Matinyi akizungumza kwenye Kongamano hilo, ameshuruku kwa zawadi hiyo ambayo amepatiwa Rais Samia, na kueleza kwamba Rais ana mapenzi ya dhati na Sekta ya habari, ndiyo maana ameshatoa maelekezo kwamba katika sheria ya huduma ya habari 2016 kwa vile vifungu ambavyo vinakandamiza uhuru wa habari vifanyiwe marekebisho.
Amesema kwa sasa wapo kwenye Mapitio ya Sera ya habari kwanza ya mwaka 2003. na Timu ya Wataalamu ipo Morogoro na kwamba mara baada ya kumaliza kufanya mapitio ya Sera hiyo, hatua inayofuata ni kufanya marekebisho ya Sheria ya huduma ya habari 2016.
“Rais Samia anaonyesha kwa dhati anapenda Sekta ya habari na sasa yupo Safarini Korea Kusini kwa ajili ya Masuala haya ya Habari, na anaunga Mkono uhuru wa habari na kujieleza na hata alipoingia Madarakani mwaka 2021 alianza kufungulia Magazeti ambayo yalikuwa yamefungwa,”amesema Matinyi.
“Kwa Ripoti zilitolewa hivi karibuni Tanzania tumeshika nafasi ya 97 kutoka 143 duniani katika uhuru wa habari na kujieleza, na kwa Nchi za Afrika Mashariki tumeshika nafasi ya kwanza, yote haya ni Matunda ya Rais Samia katika kuimarisha uhuru wa kujieleza,”ameongeza.
Aidha, amesema Serikali itaendelea kujenga Mazingira wezeshi ya Wanahabari pamoja na Taasisi zinazohusika na Taaluma hiyo katika suala zima la uhuru wa kujieleza, huku akiwataka waandishi habari wanapokuwa wakiandika habari zao, wazingatie Maadili, Sheria za Nchi, Kanuni, Uzalendo na Utu wa Mtu hasa habari za Mitandaoni.
Mkurugenzi wa MISA-TAN Elizabeth Riziki akizungumza kwenye Kongamano hilo, amesema Taasisi hiyo imefikisha miaka 30 ikijikita pia katika masuala ya uhuru wa kujieleza na imefanikiwa, na kwamba zamani kulikuwa na vyombo vya habari vichache lakini sasa hivi vipo vingi hasa vya binafsi.
Amewasihi pia wadau wa Maendeleo wafanye kazi pamoja vyombo vya habari ili kusukuma taarifa zao zifike mbali, ikiwamo kutoa elimu ya Uraia katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na uchaguzi Mkuu mwakani.
Makamu Mwenyekiti wa Misa-Tan James Marenga, amesema katika Kongamano hilo wanafanya Tafakuri ya hali ya uhuru wa kujieleza na hali ya upataji habari, hasa kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani, ili wananchi wapate haki ya kujieleza na kupata taarifa.
Nao wadau mbalimbali wa habari kutoka Ndani na Nje ya Nchi wakitoa salamu zao kwenye Kongamano hilo, wamesema Uhuru wa kujieleza ni Msingi wa haki za binadamu, na unaimarisha Demokrasia na Uwajibikaji.
Kauli Mbiu katika Kongamano hilo inasema”Uhuru wa Kujieleza ni Msingi wa Haki kwa Maendeleo endelevu”.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkurugenzi wa MISA-TAN Elizabeth Riziki akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mkurugenzi wa MISA-TAN Elizabeth Riziki akiendelea kuzungumza kwenye Kongamano hilo.
Makamu Mwenyekiti wa MISA-TAN Wakili James Malenga akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Kamishina wa Tume ya Haki na Utawala Bora Nyanda Josiah Shuli akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mwakilishi kutoka Un Human Rights East Africa Hilda Oyeua akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mwakilishi kutoka Foundation For Civil Society akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Misa Kanda Dkt. Tabani Moyo kutoka Zimbabwe akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Nacongo Rachel Chagonja akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Nacongo Rachel Chagonja akiendelea kuzungumza kwenye Kongamano hilo.
Viongozi Meza kuu wakiwa kwenye Kongamano hilo.
Washiriki wakiendelea na Kongamano.
Washiriki wakiendelea na Kongamano.
Kongamano likiendelea.
Washiriki wakiendelea na Kongamano.
Washiriki wakiendelea na Kongamano.
Washiriki wakiendelea na Kongamano.
Washiriki wakiendelea na Kongamano.
Washiriki wakiendelea na Kongamano.
Washiriki wakiendelea na Kongamano.
Washiriki wakiendelea na Kongamano.
Washiriki wakiendelea na Kongamano.
Washiriki wakiendelea na Kongamano.
Washiriki wakiendelea na Kongamano.
Makamu Mwenyekiti wa MISA-TAN Wakili James Malenga (wapili kulia)akimkabidhi zawadi ya pongezi picha ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokana na kuimarisha uhuru wa habari na kujieleza hapa nchini Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi (kushoto) kulia ni Mkurugenzi wa MISA-TAN Elizabeth Riziki.
Zawadi ya picha ya pongezi ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ikikabidhiwa.
Zawadi ya picha ya pongezi ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ikikabidhiwa.
Zawadi ya picha ya pongezi ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ikikabidhiwa.
Muonekano picha ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464