RC MACHA ASHAURI UCHUNGUZI WA KITAALAMU UFANYIKE UJENZI UKARABATI MNADA WA MHUNZE TOPE KUIBUKA JUU KUTOKA CHINI YA ARDHI
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha ameshauri uchunguzi wa Kitaalamu ufanyike katika ujenzi wa ukarabati Mnada wa Mhunze wilayani Kishapu,kufuatia kuwepo na chemchem katika eneo hilo, pamoja na Matope kuibuka juu kutoka chini ya Ardhi, ili Serikali isijeingia hasara kwa kutumia fedha nyingi.
Amebainisha hayo leo Mei 23,2024 wakati alipofanya ziara kuangalia Maendeleo ya ujenzi wa ukarabati Mnada huo wa Mhunze, kwa kujengwa ukuta wa uzio na kujionea namna chemchem iliyo huku Matope yakitoka chini ya Ardhi na kuibukia juu.
“Nisije kunukuliwa vibaya kwamba Mkuu wa Mkoa amezui ujenzi wa ukarabati wa Mnada huu wa Mhunze hapana mimi sijazuia. ili natoa ushauri tu Wataalamu waje wachunguze juu ya Tope ambalo linatoka chini ya Ardhi na hii Chemchem kama haiwezi kuleta madhara, wakisema hakuna shida basi endeleeni kujenga, wakisema litaleta shida tutafute eneo jingine ili fedha ya Serikali isije potea,”amesema Macha.
Naye Mhandisi Ahmad Abdalah kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambao ndiyo wanafanya ujenzi wa ukarabati wa Mnada wa Mhunze,amekiri ni kweli katika ujenzi huo wamepata Changamoto hiyo,na kubainisha kwamba watawapeleka Watalaamu wa Jiorojia ili kupima athari za tope hilo kama litakuwa na madhara au la ndipo waendelee na ujenzi na gharama za ujenzi wake ni Sh.milioni 710.
Nao baadhi ya wauzaji wa Mifugo kwenye Mnada huo, wamelalamikia tope hilo kwamba Mifugo yao mara nyingi imekuwa ikizama na hivyo kutumia gharama kubwa kuitoa ndani ya tope, na kwamba hata wao pia limekuwa likihatarisha usalama wao.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiwa katika Mnada wa Mhunze wilayani Kishapu akiangalia tope ambalo linaibuka juu kutoka chini ya Ardhi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiwa katika Mnada wa Mhunze wilayani Kishapu akiangalia tope ambalo linaibuka juu kutoka chini ya Ardhi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiwa katika Mnada wa Mhunze wilayani Kishapu Msingi ambao umechimbwa kwa ajili ya kujenga ukuta huku kukiwa na Chemchem ya Maji.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiwa katika Mnada wa Mhunze wilayani Kishapu akiangalia Msingi wa ujenzi wa ukuta.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof; Siza Tumbo akipiga picha maeneo ambayo yanaibuka tope kutoka chini ya Ardhi katika Mnada wa Mhunze wilayani Kishapu.
Muonekano wa Tope ambalo linaibuka kutoka chini ya Ardhi na kuja juu katika Mnada wa Mhunze wilayani Kishapu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha (kushoto)akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude katika Mnda wa Mhunze.
Mkuu wa Mkoa Anamringi Macha akiwa katika Mnada wa Mhunze wilayani Kishapu.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha (kushoto)akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude katika Mnda wa Mhunze.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiwa katika Mnada wa Mhunze wilayani Kishapu.
Viongozi mbalimbali wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha katika Mnada wa Mhunze wilayani Kishapu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464