SPIKA TULIA NA WAZIRI NAPE,WAUMIZWA NA HALI YA UCHUMI WA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA
Vyombo vya habari Tanzania vina changamoto ya kiuchumi inayo athiri hali ya ukuajia wa uhuru wa vyombo vya habari kwa kushidwa kujiendesha na hata baadhi ya vyombo kusitisha shughuli zake.
Akieleza hayo leo Mei 2,2024 Jijini Dodoma katika Maadhimisho ya siku 2 ya Uhuru wa vyombo vya habari Tanzania, Spika wa Bunge ,Tulia Akson,amesema,Uhuru wa vyombo vya habari unategemea na hali ya uchumi wa vyombo vya habari ili kuweza kukuza na demokrasia ya nchi.
Tulia amesema ili vyombo vya habari kuwa na uhuru ni vyema changamoto ya kiuchumi ya vyombo vya habari kutatuliwa ili kuweza kukuza na kuendeleza demokrasia ya nchi.
" Niagiza taasisi zote za serikali kuchukua hatua ya kulipa madeni yote ambayo wanadaiwa na vyombo vya habari na pia kuhakikisha taratibu zinafanywa kwa ajili ya watumishi wa vyombo vya habari kulipwa Mishahara yao kama watumishi wengine"Amesema Tulia.
"Uchumi wa vyombo vya habari ukiwa duni una athiri hali ya ustawi wa demokrasia kwa kuwa baadhi ya vyama vya siasa kushidwa kugharamia vyombo vya habari na waandishi kipindi cha uchaguzi"
Vyombo vya habari ,Tanzania vinasheria miaka 30 ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo habari huku vikiangaziwa kuzingatia maadili katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Aidha,Tulia amesema serikali iko tayari kupokea mrejesho kwa wadau wa habari juu changamoto za kisheria zilizo kikwazo kwa vyombo vya habari ilizifanyiwe kazi.
"Bunge kupitia kamati yake ya masuala ya sheria itafanyia kazi baadhi ya vifungu vinavyo onekana kuwa ni changamoto ya ustawi wa vyombi vya habari"amesema Tulia.
Kwa upande wake Waziri wa Habari na Mawasiliano Mhe.Nape Nauye amesema hali ya sasa ni nzuri tofauti na tulipotoka na suala llilobaki ni changamoto ya uchumi wa vyombo vya habari.
"Hatujafika tunakotaka ila mabadiliko ni makubwa kwa serikali kushirkiana na vyombo vya habari na tumefanyia kazi maboresho ya sheria kadhaa"amesema Nape.
"Hatupo tulipokuwa jana kwa sasa uhuru wa vyombo vya habari unaimarika kila siku,vyombo vya habari vinafanyakazi na ukomavu umekuwepo kwa sekta ya habari ila
hatujafuka tunapotaka kwenda"
Naye ,Rais wa Umoja wa Klabu za Habari Tanzania ,Deogratius Nsokolo akishukuru serikali kwa kufanya marekebisho ya vifungu vya sheria vilivyokuwa vina kandamiza uhuru wa vyombo vya habar Tanzania.
Waandishi wa habari Tanzania walikabiliwa na madhira kadha katika majukumu yao yaliyonyima uhuru wa habari kwa miaka 10,Matukio yaliweza kuishusha Tanzania katika sura ya kimataifa. Kwa mfano, katika ripoti za World Press Freedom Index, Tanzania iliendelea kushuka katika viwango vya uhuru wa habari kutoka nafasi ya 70 mwaka 2013 mpaka nafasi ya 124 mwaka 2021 na mwaka 2022 nafasi ya 123.
Takwimu za Baraza la Habari Tanzania za mwaka 2022,zilibainishwa taasisi zilizoongoza kwa matukio mengi dhidi ya uhuru wa habari ilikuwa ni polisi ambayo ilikuwa na matukio 51.Wahusika wengine ni pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) matukio 21, wizara mbali mbali matukio 14, wakuu wa wilaya matukio tisa, mashabiki wa mpira matukio matano, wakulima na wafugaji matukio mawili na watu wasiojulikana matukio kumi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464