Na Mapuli Misalaba
Wanafunzi wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Shinyanga kozi ya uuguzi na ukunga jana wameadhimisha siku hiyo kwa kutoa zawadi mbalimbali katika Hospitali ya Kolandoto ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wauguzi na wakunga Duniani ambapo huadhimishwa kila Mwaka ifikapo Mei 12.
Wanafunzi hao pamoja na mambo mengine wametembelea na kutoa msaada katika Hospitali ya Kolandoto kama sehemu ya maadhimisho na kumbukumbu ya siku ya wauguzi na wakunga Duniani.
Msaada huo ni Sabuni za unga, Sabuni za kipande pamoja na Mafuta vimetolewa katika Wodi ya wazazi pamoja na chumba Cha wagonjwa Hospitali ya Kolandoto.
Akizungumza katika hafla hiyo mkuu wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Paschal Shiluka pamoja na mambo mengine amewapongeza wanafunzi wa chuo hicho kwa kushiriki na kutambua umuhimu wa siku ya wauguzi na wakunga.
“Niwapongeza sana kwa kuona umuhimu wa kuadhimisha siku hii na niwapongeza wanafunzi kwa kutambua umuhimu wa kozi yenu kwamba imeanzia wapi na sasa hivi tunaposherehekea matunda ya dada yetu Florence Nightingale alikuwa mwanamke aliyechangia sana unesi wa kisasa, kwa ufupi tu niwaambie taaluma ya uuguzi na ukunga niya kitaifa na kimataifa masomo yote mnayoyasoma kwa sasa siyo tu ya kuishia hapa nchini hii ni mpaka kimataifa”.amesema Shiluka
Mkuu wa Idara ya uuguzi na ukunga katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Mwalimu Wande Kaeji ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza wanafunzi hasa wa kozi hiyo kuendeleza moyo wa majitoleo katika maeneo mbalimbali bila kujali uwezo wa mtu.
“Mimi nawaomba tu wanafunzi hawa ambao tunawafundisha na badae wataingia kutoa huduma kwenye jamii nawaomba waendelee kutoa huduma kwa moyo wa upendo lakini pia kwa kutokujali huyu ni maskini au ni tajiri na kawaida sisi wauguzi tunatoa huduma zetu kwa moyo mmoja na kwakujitolea kwa sababu tunajua kazi ya uuguzi ni wito”.amesema Mwalimu Wande.
Katika Risala ya wanafunzi wa kozi ya uuguzi na ukunga chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto ambayo imesomwa na Shufaa Said Tumkumbe amesema wameguswa kusherehekea siku ya wauguzi na wakunga Duniani kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kushiriki katika ibada ya maombi maalum, kuona wagongwa kwenye wodi katika Hospitali ya Kolandoto na kuwapatia maadhi ya mahitaji ikiwemo Sabuni na Mafuta.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kolandoto Dkt. Joseph Wallace Sahan amekishukuru chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kwa kutoa msaada huo kwa wagonjwa.
“Nawashukuru na kuwapongeza wauguzi wanafunzi wa chuo cha Sayansi za Afya kwa namna ambavyo wameendelea kuifanya kazi ya uuguzi katika Hospiatali yetu bega kwa bega pamoja na sisi lakini pia uongozi nawashukuru sana kwa zawadi mbalimbali ambazo wamezitoa siku ya leo kwa wagonjwa ambao wako mawondini zawadi hizi si chochote lakini zinaleta faraja na kuonyesha tu kwamba ishara ya upendo kwa wagonjwa ambao tunawahudumia na kwa hivyo inaleta faraja pia kwao tuko pamoja nao katika maumivu ambayo wanayoyapitia”.amesema Dkt. Sahan
Maadhimisho ya siku ya wauguzi na wakunga Duniani yameongozwa na kauli mbiu inayosema “Muuguzi sauti ya kuongoza wekeza katika uuguzi na heshimu haki za kupata afya ya kimataifa”.
Muuguzi ni mtaalam wa afya aliyeandaliwa kupitia mfumo maalum na thabiti wa kitaaluma kisha kuthibitishwa na kuidhinishwa (na mamlaka iliyopo kisheria au chombo kinachosimamia taaluma hiyo) kutoa huduma za afya.
Kaimu Muuguzi Mkuu Hospitali ya Kolandoto, Gloria Gabriel Pallangyo akiwashukuru na kuwapongeza wanafunzi wa kozi ya uuguzi na ukunga chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kwa kuwatembelea na kutoa msaada katika wodi ya wazazi pamoja na chumba cha wagonjwa.
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Kolandoto Dkt. Joseph Wallace Sahani akipongeza na kushuru kwa msaada na ushirikiano mzuru uliopo kati yao na chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto.
Baadhi ya walimu wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto wakiwa katika hafla ya kusherehekea siku ya wauguzi na wakunga.
MC Josephine Charles ambaye pia ni mtumishi katika chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto akizungumza kwenye hafla hiyo ya kuadhimisha siku ya wauguzi na wakunga Duniani.
Mkuu wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto Paschal Shiluka akizungumza ambapo amesema chuo hicho kitaendelea kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi hasa wa kozi ya uuguzi na ukunga ili kuwaimarisha wanafunzi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464