CHAD: JENERALI MAHAMAT IDRISS DEBY ITNO KUAPISHWA RASIMI KUWA RAIS

 CHAD: JENERALI MAHAMAT IDRISS DEBY ITNO KUAPISHWA RASIMI KUWA RAIS

Nchini Chad, Jenerali Mahamat Idriss Deby Itno, ambaye ameongoza serikali ya kijeshi kwa kipindi cha miaka mitatu sasa, anatarajiwa kuapishwa baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais amabao ulisusiwa na vyama vya upinzani.

Deby alitangazwa mshindi baada ya kupata asilimia 61 ya kura zote katika uchaguzi huo mwa tarehe sita ya mwezi Mei.
Deby alitangazwa mshindi baada ya kupata asilimia 61 ya kura zote katika uchaguzi huo mwa tarehe sita ya mwezi Mei. AFP - ISSOUF SANOGO

Deby alitangazwa mshindi baada ya kupata asilimia 61 ya kura zote katika uchaguzi huo mwa tarehe sita ya mwezi Mei.

Licha ya ushindi huo, mashirika yasio ya kiserikali ya kimataifa yalielezea uchaguzi huo kama usiokuwa wa haki na huru, matamshi yalioungwa mkono na mpizani wake mkuu.

Deby alitangazwa kuwa rais wa serikali ya mpito mwezi Aprili mwaka wa 2021 na kamati ya kijeshi ya maofisa 15 kufuatia kifo cha babake rais Idriss Deby Itno, aliyepigwa risasi na waasi baada ya miaka 30 madarakani.

Upinzani nchini Chad unasema uchaguzi huo wa urais haukufanyika kwa uhuru na haki.
Upinzani nchini Chad unasema uchaguzi huo wa urais haukufanyika kwa uhuru na haki. AFP - ISSOUF SANOGO

Kuapishwa kwake kunamaliza rasimi kipindi cha miaka mitatu cha uongozi wa kijeshi katika taifa hilo, hatua inayotajwa kuwa muhimu kwa vita dhidi ya makundi ya kijihadi katika ukanda wa Sahel.

Mwaka wa 2021, Deby aliidhinishwa na jamii ya kimataifa ikiongozwa na Ufaransa ambayo katika siku za hivi karibuni, vikosi vyake vimelazimika kuondoka katika mataifa yanayoongozwa na jeshi ikiwemo  MaliBurkina Faso na Niger.

Waziri Mkuu Succes Masra, mmoja wa wapinzani wakuu wa Deby kabla ya kuchukua wadhifa huo tayari ametangaza kujiuuzulu kutoka kwa wadhifa huo baada ya kuhudumu kwa miezi minne peke.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464