Kijana Tyler Thompson, mwenye umri wa miaka 21, wa Utah, ambaye ametambuliwa kuwa mmoja wa Wamarekani walioripotiwa kuhusika katika njama ya mapinduzi yaliyoshindikana huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. (AP)
Familia ya Mmarekani aliyetiwa mbaroni katika jaribio la mapinduzi lililofeli nchini Congo ilisema mtoto wao wa kiume alikuwa barani Afrika kwa mapumziko na marafiki wa familia na hakuwahi kujihusisha na harakati za kisiasa, kulingana na taarifa iliyotolewa kwa Associated Press.
Familia ya Mmarekani aliyetiwa mbaroni katika jaribio la mapinduzi liilofeli nchini Congo ilisema mtoto wao wa kiume alikuwa barani Afrika kwa mapumziko na marafiki wa familia na hakuwahi kujihusisha na harakati za kisiasa, kulingana na taarifa iliyotolewa kwa Associated Press.
Tyler Thompson alikuwa mmoja wa Wamarekani watatu ambao walitajwa na jeshi la Congo kama sehemu ya walioshiriki katika jaribio la mapinduzi lililoshindikana huko Kinshasa mapema Jumapili chini ya Christian Malanga aliyekuwa akiishi uhamishoni. Wamarekani wengine wawili wanaodaiwa kuhusika ni mlanguzi wa bangi aliyewahi kuhukumiwa, Benjamin Reuben Zalman-Polun, na mtoto wa kiume wa Malanga mzaliwa wa Utah, Marcel, mwenye umri wa miaka 21, ambaye alikamatwa na vikosi vya Congo
"Tumepigwa na butwaa na kuhuzunishwa na video tulizoziona kuhusu jaribio la mapinduzi," mama wa kambo wa Thompson, Miranda Thompson, alisema katika ujumbe wa moja kwa moja kwenye mtandao wa kijamii wa X. "Hatujui jinsi alivyojiingiza katika hali hii, ambayo ni tofauti kabisa na tabia yake . Tuna hakika kwamba hakwenda Afrika na mipango ya harakati za kisiasa.
CHANZO:VOA-SWAHILI