IRAN KUFANYA UCHAGUZI WA RAIS JUNI 28

 

IRAN KUFANYA UCHAGUZI WA RAIS JUNI 28

Picha na AFP

Iran kufanya uchaguzi wa rais Juni 28

Iran imetangaza kuwa itafanya uchaguzi wa mapema wa urais mnamo Juni 28 kufuatia kifo cha Rais Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta.

Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali IRNA, tangazo la tarehe ya uchaguzi wa 14 wa rais nchini humo limekuja baada ya mkutano kati ya wakuu wa mahakama, mamlaka ya utendaji na sheria.

Usajili wa wagombea utaanza Mei 30, ripoti hiyo ilisema, ikiongeza kuwa kampeni zitafanyika Juni 12-27.

Raisi alikuwa akirejea kutoka kwa sherehe za uzinduzi wa bwawa kwenye mpaka wa Iran na Azerbaijan siku ya Jumapili wakati ajali hiyo ilipotokea, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Iran.

Kaimu rais

Ajali hiyo pia ilisababisha vifo vya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian, na vile vile vya Malik Rahmeti, gavana wa jimbo la Azerbaijan Mashariki, na Imam Ayatollah Ali Hashim wa mkoa wa Tabriz.

Mohammad Mokhber, makamu wa kwanza wa rais wa Iran, aliteuliwa kuwa kaimu rais siku ya Jumatatu baada ya kifo cha Raisi.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464