KAGAME WA RWANDA AWASILISHA OMBI LA KUWANIA URAIS KWA MUHULA WA NNE
“Nimerudi kwenye kinyang'anyiro,” Kagame alisema kwa ufupi
alipokuwa akikabidhi faili lenye nyaraka za uteuzi wake kwa mwenyekiti wa Tume
ya Kitaifa ya Uchaguzi, Oda Gasinzigwa, wakati wa kuanza rasmi kwa uwasilishaji
wa wagombea katika tume ya uchaguzi ya nchi hiyo jijini Kigali.
Kagame alikua rais kwa mara ya kwanza
mnamo 2000, na alishinda uchaguzi wa mwisho mnamo Agosti 2017 kwa muhula wa
miaka saba kwa asilimia 98.63 ya kura, kulingana na takwimu rasmi.
Kama mgombea wa chama tawala, Rwanda
Patriotic Front (RPF), Kagame anastahili kuwania tena kufuatia marekebisho ya
katiba ya 2015 ambayo yalimwezesha kugombea kwa mihula mingine mitatu.
Uungwaji mkono wa upinzani
Kagame, mwenye umri wa miaka 66, alichaguliwa
tena kama mwenyekiti wa RPF kwa asilimia 99.8 mnamo Aprili.
Anatarajiwa kushinda uchaguzi tena
baada ya vyama vikuu vya upinzani kuidhinisha uteuzi wake.
Mwezi Septemba uliopita, Kagame
aliambia jarida moja la pan-Afrika kwamba hakuwa na wasiwasi na maoni ya
Magharibi kuhusu nia yake ya kugombea tena baada ya zaidi ya miongo miwili
madarakani huku akikabiliwa na ukosoaji wa kuzuia upinzani.
Kagame alisema kile ambacho nchi za
Magharibi zinafikiri kuhusu demokrasia “si tatizo letu.”
Mpinzani kuzuiwa
Mahakama kuu ya Rwanda
mnamo Machi mwaka huu ilikataa ombi la mwanasiasa wa upinzani Victoire Ingabire
la kuondolewa marufuku ya kisheria kwa watu waliopatikana na hatia ili
kumruhusu agombee katika uchaguzi wa urais.