Header Ads Widget

JESHI LA POLISI SHINYANGA LAKAMATA DAWA ZA BINADAMU PAKTI 86 ZILIZOKWISHA MUDA WA MATUMIZI YAKE, NA PIKIPIKI 16


Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akionyesha moja ya dawa zilizomaliza muda wake

Suzy Butondo, Shinyanga press blog

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata vitu mbalimbali zikiwemo Pakti 86 za dawa za binadamu zilizokwisha muda wa matumizi yake aina ya fragiri, ikiwa ni pamoja na pikipiki 16 za wizi na zisizo na kadi.

Vifaa vingine vilivyokamatwa ni viroba 25 vya madawa ya kulevya aina ya Mirungi, Tv 01, Mzani 01, Redio 01, pombe ya moshi lita 20 pamoja na kushughulikia kesi 15 mahakamani.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi akitoa taarifa leo jumatatu Mei 27,2024, amesema vitu hivyo vimekamatwa katika kipindi cha mwezi mmoja na wiki moja kuanzia Aprili 17, 2024 mpaka Mei 27, 2024 kufuatia Ushirikiana wa Jeshi la Polisi na Jamii katika kubaini na kutanzua uhalifu kwa kufanya doria, misako pamoja na Operesheni mbalimbali.

Aidha katika kipindi hicho pia Jumla ya kes 15 zimepata mafanikio ambapo kesi 01 ya kuvunja nyumba usiku na kuiba mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka 01 na kesi moja ya kumtaja mtu mchawi mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka mmoja.

"Kesi 01 ya kupatikana na bhangi mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha kutumikia jamii miaka 03, kesi 01 ya kuvunja duka usiku na kuiba mshitakiwa amehukumiwa kifungo cha nje miezi 12, kesi 01 ya kupatikana na madawa ya kulevya mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha kutumikia jamii miaka 02, kesi 01 ya kutorosha mtoto mshtakiwa ameamriwa kulipa faini tsh 50,000/=, kesi 01 ya kupatikana na mirungi mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha miaka 02 jela.

Kesi zingine za wizi 05 za washtakiwa wamehukumiwa kifungo kati ya miezi 03 hadi miaka 03 jela, kesi 01 ya kujeruhi mshtakiwa amehukumiwa kifungo cha mwaka 01, kesi 01 ya shambulio la kudhuru mwili mshitakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka 01, kesi 01 ya kutishia kuua kwa silaha panga mshitakiwa amehukumiwa kifungo cha nje mwaka 01",amesema Kamanda Magomi.

Amesema pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kikosi cha Usalama barabarani limefanikiwa kukamata jumla ya makosa 6320 ya Usalama Barabarani ambapo makosa ya magari ni 4847 na makosa ya bajaji na pikipiki ni1473 wahusika waliwajibishwa kwa kulipa faini za papo kwa papo.
Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakichukua taarifa kwa kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi
Kamanda wa Jeshi la polisi Janeth Magomi akionyesha magunia ya milungi yaliyokamatwa
Kamanda wa Jeshi la polisi Janeth Magomi akionyesha pikipiki zilizokamatwa





Post a Comment

0 Comments