Mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu Gagi Lala akifungua kikao
Na Kareny Masasy,Ushetu
HALMASHAURI ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga imepata hati safi ambayo wameeleza inatakiwa waipate kila mwaka huku ukusanyaji wa mapato kwa vipindi vya robo ya pili na robo ya tatu vikienda vizuri.
Katika kikao cha baraza la Madiwani cha robo ya tatu ya mwaka kilichofanyika leo tarehe 23,Mei 2024 ambapo madiwani walipitia ajenda ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa mapato ambapo robo ya pili walifikia ukusanyaji kwa asilimia 104 na robo ya tatu wako hatua nzuri ya kupita lengo.
Diwani wa kata ya Kinamapula Samweli Sharifu amesema usimamizi wa ukusanyaji mapato umekwenda vizuri ukilinganisha na mwaka wa fedha 2021/2022 ambao ukusanyaji ulikuwa mbovu na kuwasababishia kupata hati chafu.
“Vikao vya
baraza la madiwani kwa mwaka ambao walipata hati chafu kila mmoja alikuwa
akitafuta nani kasababisha na majadiliano yalikuwa makali baadaye
walipata suluhisho nini kifanyike ili kuinusuru halmashauri hii”amesema Sharifu.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu Gagi Lala amesema kweli lakini hawakukata tamaa walijipanga na kuweka mikakati ya kusonga mbele na sasa wamevuka vizuri kwa ushirikiano na miradi inatekelezwa.
Mwakilishi kutoka ofisi ya katibu tawala mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Makana amewapongeza madiwani na wataalamu kwa ushirikiano ambao wanauonyesha nakufikia kupata hati safi na wajitahidi kufuta hoja zinapoibuka.
Aidha taasisi mbalimbali za serikali ziliwasilisha taarifa zao ambapo wakala wa barabara mjini na vijini (Tarura) walieleza kuanza kuzifanyia kazi barabara zilizoharibiwa na mvua kwa fedha za dharura na zile ambazo zipo kwenye mpango wa bajeti.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464