MAGWIJI WA SOKA ADEBAYOR NA AMOKACHI KUTUA ZANZIBAR

 

Magwiji wa soka Adebayor na Amokachi kutua Zanzibar







Magwiji wa soka barani Afrika, Emmanuel Adebayor, Daniel Amokachi na Amanda Dlamini ni baadhi ya majina ya juu ambayo yamethibitishwa kwa Fainali za Bara za Michuano ya Soka ya Shule za Afrika ya CAF 2024 iliyopangwa Zanzibar kati ya 21 - 24 Mei 2024.

Shirikisho la soka barani Afrika CAF lilitangaza Jumamosi kuwa vigogo hao watakuwa miongoni mwa nyota wengine wakubwa wa mchezo huo watakaoshiriki shindano hilo, la pili kufanyika.

Michuano ya CAF ya Shule za Afrika ni mashindano ya shule ambayo yanajumuisha zaidi ya nchi 44 za Kiafrika na washiriki zaidi ya 800,000 wa Wavulana na Wasichana walio chini ya umri wa miaka 15.

Kwa mujibu wa CAF, shindano hili litam,ulika nyanja nyingine pia mbali na soka.

''Shindano hili haliangazii soka pekee bali pia programu kadhaa zikiwemo Programu ya Mwamuzi Mdogo, Mpango wa Waandishi wa Habari Vijana na Uhifadhi,'' ilisema taarifa ya CAF mtandaoni.

Majina sifika katika klabu kubwa za Ulaya

Adebayor, Mchezaji Bora wa CAF wa mwaka wa 2008, aliiwakilisha Togo kwenye Kombe la Dunia la FIFA la 2006 nchini Ujerumani kwa mara yao ya pekee kwenye michuano hiyo.

Mshambulizi wa zamani wa Arsenal, Manchester City, Real Madrid, na wengine, nyota huyo wa Togo amekuwa na kazi nzuri, akicheza zaidi ya mechi 85 akiwa na Les Eperviers.

Nyota wa kandanda wa Nigeria Amokachi aliichezea Super Eagles mechi 42 za kimataifa. Alishiriki katika Kombe la Dunia la FIFA la 1994 na 1998 na alikuwa sehemu ya timu iliyoshinda Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies CAF mnamo 1994 na Michezo ya Olimpiki mnamo 1996.

Dlamini, fahari ya Afrika Kusini

Naye Amanda Dlamini, nahodha wa zamani wa Banyana Banyana (Afrika Kusini) alicheza katika mashindano mawili ya TotalEnergies CAF Women’s Africa Cup of Nations ambapo walimaliza wa tatu na wa pili mwaka wa 2010 na 2012, mtawalia.

Ni mmoja wa wanasoka wachache, katika timu ya taifa ya wanaume na wanawake kufikisha mechi 100.

Amanda Dlamini alicheza katika mashindano mawili ya TotalEnergies CAF Women’s Africa Cup of Nations ambapo walimaliza wa tatu na wa pili mwaka wa 2010 na 2012/ Picha:  Action Images / Peter Cziborra/ Reuters 

Dlamini hivi majuzi aliweka historia alipokuwa mwanamke wa kwanza kuwa sehemu ya mchango wa maoni ya ulimwengu katika Kombe la Mataifa ya Afrika la CAF la TotalEnergies Cote d'Ivoire 2023.

Caf ilisema pia majina tajik aya wenyeji Tanzania watakuwepo kupamba shindano hilo na kutoa mchango wao katika kukuza soka ya vijana Afrika.

''Pia katika orodha hiyo wamo nyota wazawa Abdi Kassim Sadalla, Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania, na Hilda Masanche, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake U17,'' ilisema taarifa ya CAF.

Mastaa hao watashiriki katika shughuli mbalimbali za kukuza na kusaidia maendeleo ya soka miongoni mwa vijana wa Kiafrika.

Fainali hizo zitawaleta pamoja wachezaji chipukizi wenye vipaji kutoka barani kote, na kuwapa jukwaa la kuonyesha ustadi na mapenzi yao kwa mchezo huo.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464