Header Ads Widget

MAHAKAMA YA ICC YAPENDEKEZA KUKAMATWA KWA NETANYAHU

 Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC, ilisema kuwa inatafuta hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Waziri wa ulinzi wa Israel na viongozi watatu wa kundi la Hamas.

Picha na Shir Torem/AFP/Getty image

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC, ilisema kuwa inatafuta hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

"Kwa msingi wa ushahidi uliokusanywa na kuchunguzwa na Ofisi yangu, nina sababu za kuridhisha za kuamini kwamba Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, na Yoav Gallant, Waziri wa Ulinzi wa Israel, wanawajibika kwa uhalifu wa kivita na uhalifu wa kivita na ubinadamu uliofanywa katika eneo la Jimbo la Palestina (katika ukanda wa Gaza) kutoka 8 Oktoba 2023," Karima Khan, mwendesha mashtaka wa ICC amesema katika taarifa.

Mashtaka ambayo ameyaorodhesha dhidi ya Netanyahu ni pamoja na:

  • Njaa kwa raia kama njia ya vita kama uhalifu wa kivita
  • Kusababisha mateso makubwa kwa kudhamiria, au majeraha makubwa kwa mwili.
  • kutendewa kikatili kama uhalifu wa kivita kinyume na kifungu cha 8 (2)(c)(i); Kuua kwa kukusudia
  • Mauaji kama uhalifu wa kivita
  • Kuelekeza mashambulizi dhidi ya raia kwa kukusudia kama uhalifu wa kivita

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya ICC, pia inatafuta hati za kukamatwa kwa watu watatu, viongozi wa kikundi cha Hamas kwa madai ya majukumu yao katika mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 nchini Israel na kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

"Kwa msingi wa ushahidi uliokusanywa na kuchunguzwa na Ofisi yangu, nina sababu za kuridhisha za kuamini kwamba Yahya Sinwar (Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu (“Hamas”) katika Ukanda wa Gaza), Mohammed Diab Ibrahim Al - Masri anayejulikana zaidi kama Deif (Kamanda Mkuu wa tawi la kijeshi la Hamas, linalojulikana kama Brigedi za Al-Qassam)," taarifa hiyo imeongezea.

"Na Ismail Haniye (Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas) wanawajibika kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu unaofanywa katika eneo la Israeli na Jimbo la Palestina (katika ukanda wa Gaza) kutoka angalau 7 Oktoba 2023," imeongezea.

Mashataka ambayo yapo dhidi yao ni pamoja na:
  • Mauaji kama uhalifu dhidi ya ubinadamu
  • Kuchukua mateka kama uhalifu wa kivita
  • Ubakaji na vitendo vyengine vya unyanyasaji wa kijinsia
  • Kuwatesa watu
  • Vitendo vya kikatili

"Ofisi yangu inakubali kwamba uhalifu wa kivita unaodaiwa katika maombi haya ulitekelezwa katika muktadha wa mzozo wa kimataifa wa silaha kati ya Israel na Palestina, na mzozo wa silaha usio wa kimataifa kati ya Israel na Hamas unaoendana sambamba," ICC imesema

CHANZO:TRT AFRIKA

Mahakama ya ICC yapendekeza kukamatwa kwa Netanyahu - TRT Afrika

Post a Comment

0 Comments