Header Ads Widget

KANISA LA PHILADELPHIA GOSPEL ASSEMBLY INTERNATION P.G.A.I LAZINDUA CHUO CHA BIBLIA SHINYANGA

Makamu Askofu wa kanisa la Philadelphia Gospel Assembly Internation ( P.G.A.I ) Baraka Laizer baada ya kukata utepe akifurahia


Na Suzy Butondo, Shinyanga


Makamu Askofu wa kanisa la Philadelphia Gospel Assembly Internation ( P.G.A.I ) Baraka Laizer amezindua jengo la chuo cha biblia na kuliweka wakfu kwa ajili ya mafunzo ya biblia, Mkoani Shinyanga.

Akizindua jengo hilo Askofu Laizer amesema jengo hilo litatumika kama darasa la kujifunza biblia, ambalo limeanza rasm May 20,2024 katika kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga mkoani hapa.

Askofu Laizer amesema chuo hicho kitaenda kuzaa matunda nchi nzima ambacho kitawaandaa wachungaji, wainjilisti, walimu mitume, manabii na maaskofu kwa ajili ya kumtumikia Mungu duniani kote.

"Katika siku ya leo wanaanza jumla ya wanafunzi 12 walioandaliwa, na awamu ya pili watatangaziwa watu kutoka sehemu mbalimbali wakati miundombinu ya mabweni, madarasa na vifaa vingine mbalimbali kukamilika, hivyo wenye uhitaji wa kujiendeleza na masomo ya biblia kwa ajili ya kufundisha watu wamjue Mungu wakae mkao wa kula, ili kazi ya Mungu iendelee kusonga mbele na watu wamjue Mungu,"amesema Askofu Laizer.

"Ili jengo hili liweze kutumika kwa ajili ya Mungu tunaliweka wakfu katika siku ya leo, ambapo wanafunzi hao wataanza masomo ya biblia katika chuo hiki, hivyo Philadelphia tunakwenda kuzaa matunda nchi nzima, ambao wataandaliwa hapa na kwenda kuzaa matunda sehemu mbalimbali za nchi,"ameongeza.

Baadhi ya wanafunzi waliojisajili katika chuo hicho kwa ajili ya kuanza masomo ya biblia akiwemo Anania Clementi na Dionisio Kaijage wamesema wanalishukuru kanisa la Philadelfia kwa kuanzisha chuo hicho ambacho kitawasaidia kujifunza biblia na kuweza kufundisha watu wengine wanaohitaji kumjua Mungu.

"Tunamshukuru Mungu kwa kumpa maono makubwa ya kuanzisha chuo hiki Makamu Askofu Laizer, kwani tulikuwa na uhitaji mkubwa wa kujifunza biblia kwa undani, lakini kwa uweza wa mwenyezi Mungu leo tunaanza rasmi katika chuo hiki kipya hivyo, tunamuomba Mungu akatuwezeshe wote tunaoanza leo na tukahitimishe wote,"amesema Clementi

Nae Mchungaji msaidizi wa kanisa la Philadelphia Miracle Temple Shinyanga Herman Hezron amesema ni jambo la kumshukuru Mungu, kwani kuanzishwa kwa chuo hiki kitatuwezesha kuwahubiri wengine kwa habari ya Mungu ili watu wengi wakaijue kweli ya Mungu.

"Vile vile tunamshukutu Mungu kwa ajili ya mchungaji wetu kiongozi ambae ametembea na maono haya kwa kipindi kirefu na sasa maono haya yanatimia na tayari masomo yameanza Mungu aendelee kumuongezea maono zaidi ili tuendelee mbele zaidi,"amesema Mchungaji Herman.
Makamu Askofu wa kanisa la Philadelphia Gospel Assembly Internation ( P.G.A.I ) Baraka Laizer akiwa na mke wake mchungaji Evaline Msangi wakizindua rasmi masomo ya biblia
Makamu Askofu wa kanisa la Philadelphia Gospel Assembly Internation ( P.G.A.I ) Baraka Laizer akiwa na mchungani msaidizi wa Hanania la Philadelfia Ndembezi manispaa ya Shinyanga akisoma neno la Mungu kabla ya kuzindua
Makamu Askofu wa kanisa la Philadelphia Gospel Assembly Internation ( P.G.A.I ) Baraka Laizer akiwa na mchungani msaidizi wa Hanania la Philadelfia Ndembezi manispaa ya Shinyanga akisoma neno la Mungu kabla ya kuzindua
Makamu Askofu wa kanisa la Philadelphia Gospel Assembly Internation ( P.G.A.I ) Baraka Laizer akiwaelekeza wanafunzi wanaoanza darasa la masomo ya bibl

Makamu Askofu wa kanisa la Philadelphia Gospel Assembly Internation ( P.G.A.I ) Baraka Laizer akiandika kwenye ubao wa chuo hicho utangulizi wa masomo ya biblia
Waumini wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple Shinyanga mjini wakifurahia baada ya jengo la chuo kuzinduliwa
Waumini wa kanisa la Philadelfia Miracle Temple Shinyanga mjini wakimsikiliza Makamu Askofu wa kanisa la Philadelphia Gospel Assembly Internation ( P.G.A.I ) Baraka Laize
Miracle kwaya ya kanisa la Philadelphia wakiwa kwenye picha ya pamoja
katika jengo la chuo cha biblia
Miracle kwaya ya kanisa la Philadelphia wakiwa kwenye picha ya pamoja katika jengo la chuo cha biblia
Jengo la chuo cha biblia lililozinduliwa



Post a Comment

0 Comments