MWENYEKITI WA UMOJA WA WANAWAKE UWT CCM SHINYANGA MJINI AWATAKA VIONGOZI KUEPUKANA NA VIVURUGE WA KUTAKA MADARAKA KABLA YA MUDA

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CCM wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye mkutano wa UWT kata ya Kizumbi

Suzy Butondo, Shinyanga press blog

Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake UWT CCM Wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo amewataka viongozi mbalimbali wa CCM kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga amewataka kuepuka vivuruge ambao wanaweza kusababisha mpasuko ndani ya chama, badala yake wawaambie bado muda wake.

Hayo ameyasema juzi kwenye mkutano wa UWT kata ya Kizumbi, wakati akiwa mgeni rasmi ambapo amesema kuna vivuruge wengi wameanza kuvuruga kwenye chama hao watu muwaepuke, kwani wanaweza kuleta mipasuko ndani ya chana chetu cha mapinduzi CCM.

"Tunatakiwa tuwaepuke watu hao wanaovuruga tunatakiwa tuwape ushirikiano wenye mashamba yao, hao wanaokuja kuvuruga tuwaambie bado muda wasubiri kengele likipigwa ndiyo watakuja mpaliliaji hana shamba, tuacheni kubeba wagombea wa pembeni tunawakatisha tamaa viongozi walioko madarakani wapeni ushirikiano viongozi wenu "amesema Nhamanilo.

Pia Nhamanilo amewataka wanawake wenye sifa wajitokeze kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali za serikali za mitaa, ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wananchi wote kujiandikisha kwenye daftari la kudumu.

"Niwaombe wazazi wote tuendelee kuwalea malezi mema watoto wetu wasijiingize kwenye makundi yasiyofaa tuwasimamie na kuwafundisha maadili mema, pia tuzungumze na watoto wetu wa kike tukemee mabaya tuwafundishe tabia njema ili baadae waweze kutimiza ndoto zao,"amesema Nhamanilo.

Diwani wa kata ya Kizumbi Reuben Kitinya amesema kata hiyo inachangamoto ya watoto wa kike kupata ujauzito, ambapo mwaka 2023 watoto 11 walipata ujauzito na mwaka huu kuanzia january mpaka sasa mwezi Mei kuna mimba tatu hivyo aliomba wilaya na mkoa isaidie ili watoto hao wasiendelee kukatishwa masomo na kwa kupata mimba mashuleni.

"Katika kata hii tuna kilio kikubwa sana kwani tumezungukwa na chuo cha Kizumbi, ambacho kina wanafunzi 860 ambapo 210 wanaishi kwenye mabweni, lakini wengine wamepanga kwenye mitaa yetu na tuna chuo cha Veta kina wanafunzi zaidi ya 600 wengi wamepanga kwenye mitaa yetu na tuna kambi ya jeshi, na kuna gulio kutokana na mkusanyika wa watu wengi, hii imekuwa ikisababisha watoto wa kike kushawishika na kuambulia ujauzito, hivyo serikali isaidie ili watoto hawa waweze kutimiza ndoto zao"amesema Reuben.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CCM wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye mkutano wa UWT kata ya Kizumbi
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CCM wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye mkutano wa UWT kata ya Kizumbi

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CCM wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye mkutano wa UWT kata ya Kizumbi

Katibu wa UWT kata ya Kizumbi Rebeka Daudi akia taarifa ya kata yake

Wajumbe mbalimbali wa mkutano huo wakiwa kwenye mkutano wa UWT kata ya Kizumbi
Wajumbe mbalimbali wa mkutano huo wakiwa kwenye mkutano wa UWT kata ya Kizumbi

Diwani viti maalumu Moshi Kanji ambaye ndiye mlezi wa kata hiyo akizungumza kwenya mkutano huo

Diwani viti maalumu wilaya ya Shinyanga Ester Makune akizungumza kwenye mkutano huo
Diwani viti maalumu wilaya ya Shinyanga Paskazia Seni akizungumza kwenye mkutano huo

Baadhi ya Madiwani viti maalumu wakiwa kwenye mkutano huo waliokuwa wamearikwa, kazi kazi

Wajumbe mbalimbali wa mkutano huo wakiwa kwenye mkutano wa UWT kata ya Kizumbi

Wajumbe mbalimbali wa mkutano huo wakiwa kwenye mkutano wa UWT kata ya Kizumbi

Wanawake wakimpokea mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga akiingia katika viwanja vya mkutano huo ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464