Diwani wa kata ya Ngokolo Victor Mkwizu akiwa kwenye mkutano wake katika mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga
Suzy Butondo Shinyanga Press blog
Diwani wa kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga Mkoani hapa Victor Mkwizu amewataka wazazi na walezi kukemea mmomonyoko wa maadili kwa watoto na kuwafundisha maadili mema watoto wao, ili wasijiingize kwenye wimbi la ushoga na usagaji.
Hayo ameyasema Mei 29, 2024 kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, ambapo alisema Wazazi wengi wamekuwa wako bize na shughuli zao na kuwacha watoto wakijichunga wenyewe hali ambayo imekuwa ikisababisha watoto wengi kutokuwa na maadili mema.
"Niwaombe wazazi wote na walezi katika kata yetu tuwasimamie watoto wetu na tuwaonye pale wanapokosea, kwani kuna tabia ambazo baadhi ya watu wanazifanya wanawahalibu watoto wakiume wanalawitiwa kwenye mapagale na watoto wa kike wanasagana hali ambayo si salama kwa kata yetu na Taifa kwa ujumla"amesema Mkwizu.
Aidha diwani Mkwizu akitoa taarifa za utekelezaji wake katika kata ya Ngokolo alieleza kutelezwa kwa ahadi zake wakati akiomba ridhaa ambazo amesimamia na zikatekelezwa kama vile Ujenzi wa soko kuu la mitumba na choo cha kisasa ambalo limekamilika na linatumika, ujenzi wa stand ndogo Soko la majengo mapya.
Mkwizu ameeleza mikopo, amesema mikopo ya wajasiriamali bado inaendelea kutolewa, urasimishaji na upimaji wa milki za viwanja vya makazi na taasisi imefanyika mitaa ya Mwadui, Mageuzi, Kalonga na Majengo mapya, pia mikakati ya kuanza ujenzi wa kituo cha afya imekamilika na taratibu za kukamilisha ujenzi na kufungua kituo cha polisi zinaendelea kwa mamlaka husika.
"Pia tumeendelea kusikiliza kero mbalimbali na kuzitatua, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kuchangia miradi ya maendeleo yenye tija, kufanya ulinzi shirikishi, tunahamasisha wazazi wote mchangie chakula mashuleni, kwani watoto wasipopata chakula hawawezi kusoma vizuri,amesema Mkwizu.
"Nawashukuru sana wananchi wangu wa kata ya Ngokolo kwa kuhudhuria mkutano huu wa kata kwa ajili ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi CCM na kuzungumzia miradi mbalimbali iliyotekelezwa ndani ya kata takribani shilingi Bilioni 1.8 ambazo zimetumika ikihusisha ujenzi wa madarasa,matundu ya vyoo" ameeleza
"Pia naishukuru serikali ya CCM inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya muungano ya Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za miradi hiyo, na namshukuru mbunge wa Jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi kwa kusimamia upatikanaji wa fedha, Mstahiki Meya wa Manispaaa na baraza la Madiwani kwa kutenga fedha kutoka mapato ya ndani na kutekeleza miradi ndani ya kata ya Ngokolo"ameongeza Mkwizu.
Mkutano huo ulihudhuliwa na mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko ambaye alijibu hoja mbalimbali za wananchi na kuelezea miradi mbalimbali iliyofanyika katika kata ya Ngokolo na manispaa kwa ujumla, ambapo aliwapongeza wananchi kwa kuzingatia usafi na kusababisha manispaa kupata ushindi mkubwa.
"Pia naomba na mimi nipigilie msumari kwenye kusimamia maadili ya watoto wetu, tuwaombe wazazi wakemee watoto wasifanye maovu na muwafundishe, tusiwaachie watoto wacheze na mitandao kwani ndiyo inayowaharibu, tusipowaonya tunaangamiza Taifa"amesema Masumbuko.
Kwa upande wake mtendaji wa kata ya Ngokolo Gaudiozi Mwombeki amesema katika kata hiyo kumetokea mmomonyoko wa maadili kwa jinsia zote na kuathiri watoto wadogo, hivyo aliomba lipigwe vita na halikubali ndani ya jamii ya watanzania.
"Pia alisema shughuli za maendeleo katika kata ya Ngokolo zinaendelea kutekelezwa kwa kuchongwa barabara,kujenga mitaro pamoja na makalvati kwa mitaa yote saba ya kata ya Ngokolo na baadhi ya barabara zimekamilika, na baadhi bado kuna uhitaji mkubwa wa barabara, miradi hii inatekelezwa chini ya usimamizi wa ofisi ya Tarura"amesema. Mwombeki
Viongozi mbalimbali wa kata ya Ngokolo wakimsikilza Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko
Diwani wa kata ya Ngokolo Victor Mkwizu akiwasikiliza wananchi wakitoa kero zao mbalimbali
Viongozi mbalimbali wa kata ya Ngokolo
Wananchi wa kata ya Ngokolo wakiwa kwenye mkutano wa diwani
Wananchi wa kata ya Ngokolo wakiwa kwenye mkutano wa diwani
Wananchi wa kata ya Ngokolo wakiwa kwenye mkutano wa diwani
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464