Header Ads Widget

WAKALA WA VIPIMO MKOANI SHINYANGA WATAKA WANANCHI WAPATE VIPIMO SAHIHI KATIKA DIRA ZA MAJI




Maafisa kutoka Wakala wa vipimo mkoani Shinyanga wakikagua mita au dira za maji katika gati

Na Kareny  Masasy,Shinyanga
 

WAKALA wa vipimo (WMA) mkoani Shinyanga imekagua dira za maji   kwenye ghati na majumbani katika kata ya Chibe lengo kujirizisha na matumizi sahihi   ya vipimo vya dira za maji.

Hayo yamesemwa leo tarehe 20/Mei/2024  na Afisa mwandamizi wa wakala wa Vipimo mkoa Leo Thadey katika kuazimisha siku ya vipimo duniani  yenye kauli mbiu tunapima Leo kwa kesho endelevu ambapo alisema  wamechukua jukumu la kupima dira za maji kwa mujibu wa Sheria sura 340.

Thadey amesema  mita zinatakiwa zitolewe na wasambazaji (Suplier)  na kila baada ya miaka miwili  zikaguliwe na kupimwa  na ndiyo Leo wameamua   kutoa  elimu kwa  wananchi kwa vitendo  upande wa dira za majumbani.

 Afisa mwandamizi kutoka WMA mkoa wa Shinyanga Happiness Saronge amesema  Chibe kuna gati 14 zinayosambaza maji  na wananchi  Sasa wafahamu wakala wa Vipimo jukumu lao ni nini hasa huku wakitakiwa  kupata  vipimo vilivyo sahihi na kile wanachokilipia na wafahamu dira zote zinapimwa.

Afisa Vipimo  Masoud  Thiney amesema  lengo  Vipimo lazima vifuatwe  kwa mujibu wa Sheria na taratibu  na tunapima dira zote za maji zinazotumiwa na jamii.

“Mkoa unatekeleza kwenda kupima na tuko kata ya chibe  kwa kwa kuangalia  changamoto kwani baadhi ya wakazi walikuwa wakilalamika  mita hivyo tumechukua jukumu la  kuzicheki kama kweli ni mita au ni miundombinu”amesema Thiney.

Mtendaji wa Mtaa wa Chibe  Joseph Kija amesema  mradi wa maji unasimamiwa na  Wakala wa maji na mazingira vijijini  (Ruwasa) na wasimamizi wa gati walidai bili zinazotoka  ni kubwa  kupitia wakala wa Vipimo malalamiko yataondoka tatizo limebainika baada ya kuzipima.

 Maafisa vipimo wakikagua mita mtaa wa ChibeMaafisa wakikagua  vipimo Mtaa wa Chibe Manispaa ya Shinyanga

Mkazi wa Chibe akichota maji kwenye gati

Maafisa wakikagua mita ya maji katika gati





Post a Comment

0 Comments