WATOTO NGOKOLO WAANIKA CHANGAMOTO WANAZOKUMBANA NAZO SHULENI

Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akizungumza wakati akifungua kikao cha Watoto wa Baraza la Watoto Kata ya Ngokolo na Watoa Maamuzi Ngazi ya Kata na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 

Na Kadama Malunde -  Malunde 1 blog

Shirika la Rafiki SDO limekutanisha Watoto wa Baraza la Watoto Kata ya Ngokolo na Watoa Maamuzi Ngazi ya Kata na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kutengeneza Kadi alama na mpango kazi wa utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Asasi za Kiraia (MKUA) ambapo watoto wamewasilisha changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo shuleni.

Kikao hicho kimefanyika leo Jumamosi Mei 11,2024 katika ukumbi wa ofisi ya Shirika la Rafiki SDO uliopo kata Kitangili Manispaa ya Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban.

Meneja Mradi wa Kukuza Asasi za Kiraia (MKUA) , Maria Maduhu kutoka Shirika la Rafiki SDO amesema lengo la kikao hicho ni kutengeneza kadi alama (Viashiria na changamoto wanazopitia watoto) na kutengeneza mpango kazi wa kutatua changamoto zilizobainika katika shule nne ambazo ni shule ya Msingi Mapinduzi A na B, shule ya msingi Mwadui na Shule ya Sekondari Ngokolo zilizopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Ameeleza kuwa kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Asasi za Kiraia (MKUA) ambapo kwa Rafiki SDO unalenga kuimarisha mabaraza ya watoto ili kutetea haki zao na kujua wajibu wao na kwamba Rafiki SDO itafanya ufuatiliaji wa mpango kazi uliotengenezwa ambapo watoa maamuzi watafanya utekelezaji wa kutatua changamoto zilizojitokeza.

“Rafiki SDO inatekeleza mradi wa MKUA katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Shinyanga na Manispaa ya Kahama. Huu ni mradi wa miaka mitatu 2022-2024”,ameongeza.

Kikao hicho kimekutanisha Watoto wa baraza la watoto la Ngokolo na Watoa Maamuzi ngazi ya kata ya Ngokolo na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Miongoni mwa viashiria na changamoto wanazokabiliana nazo watoto shuleni ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kusomea na kujifunzia ikiwemo vitabu ambapo wamedai sasa hivi watoto watano wanalazimika kutumia kitabu kimoja hali inayosababisha washindwe kufanya mazoezi ya kazi walizopewa darasani.

Changamoto nyingine ni ukosefu wa umeme, upungufu wa madawati hali inayopunguza utulivu wa wanafunzi darasani lakini pia upungufu wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo katika shule za msingi na vyoo upande wa shule ya Sekondari Ngokolo upande wa wavulana havitoshi, ukosefu wa chumba maalum cha kujistiri katika shule ya Sekondari Ngokolo.

Kwa upande wa idadi ya walimu watoto hao wamesema hali hairidhishi mfano katika shule ya Sekondari Ngokolo kuna mwalimu mmoja pekee wa Sayansi licha ya kwamba wanafunzi ni wengi ambapo kuna mkondo A hadi H.

Wamezitaja changamoto zingine ni ukosefu wa mambomba ya maji kwenye vyoo, ukosefu wa maktaba, ukosefu wa walimu wa wanafunzi wenye mahitaji maalum, ukosefu wa vifaa vya michezo, elimu ya utengenezaji sodo pamoja na shule kutokuwa na uzio hali inayosababisha mifugo kuingia shuleni na kuharibu mimea.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa amelishukuru na kulipongeza shirika la Rafiki SDO kwa kutengeneza mabaraza ya watoto na kuwajengea uwezo watoto hali inayosababisha wajiamini na kuweza kutetea haki zao.

Diwani wa Kata ya Ngokolo amesema serikali inaendelea kutatua changamoto za wananchi ikiwemo kujenga miundombinu ya shule yakiwemo madarasa na matundu ya vyoo.
Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akizungumza wakati akifungua kikao cha Watoto wa Baraza la Watoto Kata ya Ngokolo na Watoa Maamuzi Ngazi ya Kata na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumamosi Mei 11,2024 katika ukumbi wa Ofisi ya Rafiki SDO Kitangili Manispaa ya Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akizungumza wakati akifungua kikao cha Watoto wa Baraza la Watoto Kata ya Ngokolo na Watoa Maamuzi Ngazi ya Kata na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 
Diwani wa Kata ya Ngokolo Mhe. Victor Mkwizu akizungumza wakati wa kikao cha Watoto wa Baraza la Watoto Kata ya Ngokolo na Watoa Maamuzi Ngazi ya Kata na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 
Diwani wa Kata ya Ngokolo Mhe. Victor Mkwizu akizungumza wakati wa kikao cha Watoto wa Baraza la Watoto Kata ya Ngokolo na Watoa Maamuzi Ngazi ya Kata na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 
Meneja Mradi wa Kukuza Asasi za Kiraia (MKUA) , Maria Maduhu kutoka Shirika la Rafiki SDO akizungumza wakati wa kikao cha Watoto wa Baraza la Watoto Kata ya Ngokolo na Watoa Maamuzi Ngazi ya Kata na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 

Wanafunzi wakiwasilisha changamoto wanazokabiliana nazo shuleni wakati wa kikao cha Watoto wa Baraza la Watoto Kata ya Ngokolo na Watoa Maamuzi Ngazi ya Kata na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 
Wanafunzi wakiwasilisha changamoto wanazokabiliana nazo shuleni wakati wa kikao cha Watoto wa Baraza la Watoto Kata ya Ngokolo na Watoa Maamuzi Ngazi ya Kata na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga 
Watoa Maamuzi Ngazi ya Kata ya Ngokolo na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga  wakiwa ukumbini
Watoa Maamuzi Ngazi ya Kata ya Ngokolo na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga  wakiwa ukumbini
Watoto wakifuatilia matukio ukumbini
Watoto wakifuatilia matukio ukumbini
Watoto wakifuatilia matukio ukumbini
Watoto wakifuatilia matukio ukumbini
Watoto wakifuatilia matukio ukumbini
Watoa Maamuzi Ngazi ya Kata ya Ngokolo na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakifanya majadiliano

Mijadala ikiendelea
Mijadala ikiendelea

Mmoja wa watoto akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Mmoja wa watoto akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Mmoja wa watoto akichangia hoja wakati wa kikao hicho
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464