WFP YATAHADHARISHA JUU YA KUONGEZEKA KWA NJAA

 WFP imesema jana kwamba hali mbaya ya hewa inayohusishwa na hali ya hewa ya El Nino inasababisha kuongezeka kwa njaa katika nchi kadhaa, zikiwemo Zambia na Afghanistan na kutoa wito wa msaada kutoka kwa wafadhili.

Picha: Sascha Steinach/dpa/picture-alliance

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula WFP limesema jana kwamba hali mbaya ya hewa inayohusishwa na hali ya hewa ya El Nino inasababisha kuongezeka kwa njaa katika nchi kadhaa, zikiwemo Zambia na Afghanistan na kutoa wito wa msaada kutoka kwa wafadhili.

Katika taarifa, WFP imeonya kuwa eneo la Kusini mwa Afrika ni '' kitovu cha mgogoro" baada ya mafuriko na ukame kukumba eneo hilo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Soma pia: WFP: Mvua imesababisha vifo vya watu 300 Afghanistan

WFP imesema mataifa matatu ya Malawi, Zimbabwe na Zambia, ndio yaliyoathirika zaidi na kushuhudia kati ya asilimia 40-80 ya mazao yao makuu ya mahindi yakiharibika kutokana na ukame wa msimu huu na kuathiri mamilioni ya watu.

Katika taarifa, mkurugenzi mtendaji wa WFP Cindy McCain aliyesafiri hadi Zambia na kujionea hali ilivyo, amesema familia nchini humo zinahitaji sasa msaada huku wakiendelea kuweka mikakati ya kukabiliana na hali hiyo katika siku zijazo.

CHANZO:DW-SWAHILI

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464