WANAWAKE UWT CCM MKOA WA SHINYANGA WAFUNDWA


Afisa wa idara ya Organaizesheni kutoka UWT makao makuu Taifa Sophia Nyalusi akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa UWT Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Suzy Butondo, Shinyanga press blog

Wanawake wa UWT CCM Mkoa wa Shinyanga wametakiwa kupendana na kujitokeza kwa wingi katika kugombea nafasi mbalimbali za serikali za mitaa, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu.

Agizo hilo limetolewa leo 22,2024
na afisa wa idara ya Organaizesheni UWT CCM kutoka makao makuu Taifa Sophia Nyalusi kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa UWT Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Nyalusi amesema uchaguzi wa serikali za mitaa umekaribia ni vizuri wananchi wakahamasishwa katika kujiandikisha kwenye daftari la kudumu , ili waweze kushiriki katika kupiga kura, kwani wasipojiandikisha hawawezi kupiga kura.

"Niwaombe sana wanawake wenzangu tuwahamasishe wananchi wote wajiandae kujitokeze kwa wingi katika kujiandikisha kwenye daftari la kudumu, pia muwahamasishe na wanawake wajitokeze katika kugombea nafasi mbalimbali za serikali za mitaa,"amesema Nyalusi.

Kwa upande wake katibu msaidizi wa CCM mkoa wa Shinyanga Halima Makoroganya amesisitiza wanawake wapendane na kushirikiana kwa pamoja katika kukijenga chama cha Mapinduzi na jumuiya zake ili kuhakikisha chama kinaendelea kushika dola.

"Naomba nisisitize tena kwamba ili wanawake tuweze kufanya mambo makubwa kwa ajili ya kukijenga chama chetu na kuleta maendeleo katika mkoa na Taifa kwa ujumla ni lazima tupendane na tuwe wamoja nina imani tutafanya mambo makubwa kwa sababu tunaweza,"amesema Makoroganya.

Naye Mjumbe wa baraza la UWT Taifa Christina Gule amewataka viongozi wote kuwaibua wanawake waweze kuchukua Form za kugombea nafasi za serikali za mitaa, kwani kuna nafasi mbalimbali ambazo wanaweza kuomba.

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga Grace Bizulu amewataka wanawake kuwa na ushirikiano ili kuhakikisha chama cha mapinduzi kinaendelea kushila dola, katika chaguzi za serikali za mitaa.

Afisa wa idara ya Organaizesheni kutoka makao makuu Taifa Sophia Nyalusi akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa UWT Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Afisa wa idara ya Organaizesheni kutoka makao makuu Taifa Sophia Nyalusi akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa UWT Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga Grace Bizulu akizungumza kwenye mafunzo hayo
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala akifurahia baada ya kumaliiza mafunzo hayo
Mjumbe wa baraza UWT Taifa Christina Gule akizungumza
Katibu msaidizi wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Halima Makoroganya akizungumza kwenye mafunzo hayo
Viongozi wa UWT mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja baaa ya kumaliza mafunzo
Viongozi wa UWT mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja baaa ya kumaliza mafunzo
Viongozi wa UWT mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja baaa ya kumaliza mafunzo
Viongozi wa UWT mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye picha ya pamoja baaa ya kumaliza mafunzo






































Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464