Header Ads Widget

ALIYEUA MWANAE KWA KUMNYONGA KISA HAJAFANANA NAYE AHUKUMIWA KUNYONGWA.

 

   Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Geita

    Salum Maige, Geita.20/06/2024

 MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Geita imemhukumu mkazi wa kijiji cha Masumbwe wilayani Mbogwe Shemas Juma adhabu ya kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa kukusudia mtoto wake Anna Shemas  mwenye umri wa mwezi mmoja.

 Mshitakiwa huyo katika kesi namba 53 ya mwaka 2022 alikuwa anakabiliwa na kesi ya mauaji ya mwanae ambapo mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Oktoba 19,mwaka 2021 kwa madai ya kwamba mtoto huyo alizaliwa akiwa hajafanana naye.

 Akitoa hukumu hiyo Juni 19,2024 Jaji mfawidhi wa Mahakama hiyo Kelvin Mhina amesema upande wa mashtaka umethibitisha pasi na shaka kuwa mshtakiwa alimuua Anna Shemas kwa kukusudia kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

 Akisoma hukumu hiyo Jaji Mhina ameeleza kuwa Mahakama umetoa uamzi huo kwa kuzingatia  ushahidi wa pande zote mbili uliotolewa mahakamani hapo na kuthibitishwa kwamba kweli kifo cha mtoto huyo kilikuwa sio cha kawaida na kweli mshtakiwa huo alihusika.

 Katika kesi hiyo upande wa serikali uliongozwa na mawakili wawili Godfrey Odopoy na Kabula Benjamini ambao katika mahakama hiyo kutokana na ushahidi uliotolewa waliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine yenye nia ya kutenda kosa kama hilo.

 Awali,katika kesi hiyo upande wa serikali ulikuwa na mashahidi wanane pamoja na vielelezo viwili ikiwemo hati ya uchunguzi wa daktari na maelezo ya upande wa ofisi ya upelelezi wa makosa ya jinai.

 Katika mwenendo wa kesi hiyo ushahidi ulitolewa na mganga wa kituo cha Afya Masumbwe ulionyesha kuwa mtoto huyo alifariki kwa kukosa pumzi,hivyo alifariki aidha kwa kunyongwa au kubanwa pumzi na uchungiz huo ulifanywa baada ya mwili wa mtoto kukutwa kwenye dimbwi la maji ukiwa umeharibika huku ukiwa unatoa harufu.

 Baada ya ushahidi huo pamoja na ushahidi mwingine uliotolewa katika mwenendo wa kesi hiyo mahakama kuu kanda ya Geita chini ya Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo Kelvin Mhina imemtia hatiani na kumhukumu bwana Shemasi Juma adhabu kifungu cha kunyongwa hadi kufa.

 

Post a Comment

0 Comments