TUMIENI MAFUNZO HAYA KUONGEZA TIJA YA KAZI ZENU - HILDA.
Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MRAJIS Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga B. Hilda Boniphace amewataka viongozi na washiriki wa Bodi za Vyama vya Ushirika vya Mazao ya Bustani (HORTCULTURAL AMCOS) ambao wameanza mafunzo ya siku mbili katika Ukumbi mdogo wa Mikutano uliopo Lyakale Hotel kuyatumia vizuri mafunzo haya ili yakalete tija zaidi katika utekelezaji wa shughuli zao huku akisisitiza ifike wakati waondokane na soko la ndani peke yake, waweze kuzalisha zaidi na kusafirisha nje ya nchi kwani wanao uwezo huo.
Hilda ameyasema haya leo tarehe 3 Juni, 2024 alipokuwa akifungua mafunzo haya yaliyojumuisha viongozi 18 ambao wamekuwa wakishughulika na kilimo cha mbogamboga na matunda katika Kijiji cha Bugalama, Kata ya Bugalama Halmashauri ya Wilaya ya Msalala na kuhudumia Mgodi wa Bulyanhulu kupitia
"Twendeni tukayatumie vizuri mafunzo haya ili yalete tija na kuleta ubunifu wenye kuinua uchumi wa mmoja mmoja na Uahirika kwa ujumla katika kutekeleza shughuli zenu za kilimo cha mbogamboga na matunda, kwani uwezo huo mnao na Serikali imefungua fursa zaidi katika kuuza bidhaa hizi nje ya nchi," amesema Bi. Hilda.
Bi. Hilda amesema kuwa Vyama vya Mazao ya Bustani ni vichache sana, na kwakuwa wao wameonesha uwezo mkubwa katika kuhudumia Mgodi ni wakati wao sasa kwenda kuboresha zaidi mara baada ya mafunzo haya na ndiyo lengo kuu la mafunzo haya wanayopatiwa na ukizingatia kuwa hata Serikali imetilia mkazo mkubwa zaidi kilimo cha matunda na mbogamboga ambapo Wanaushirika au kikundi waweza kunufaika zaidi.
Kwa upande wake Ndg. Justin Mogendi ambaye ni muwezeshaji na mtoa mada kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika - Dodoma amsema kuwa Serikali imejipanga vizuri sana kuhakikisha kuwa biashara ya zao la mbogamboga na matunda linaimarika zaidi ndani na nje ya nchi na ndiyo sababu hata wao pamoja na wadau wengine wamekutana hapa.
Katika Mafunzo haya mada mbalimbali zitafundishwa na Justin Mogendi - TCDC, Spania Nyobuya - TCDC, Justine Mallo - COASCO SHINYANGA, Laurent Mikama - TAMISEMI na Mafy Tickin - MoCU SHINYANGA.