Header Ads Widget

MWENYEKITI UVCCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI JONATHAN MADETE ATUMBULIWA

MWENYEKITI UVCCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI JONATHAN MADETE ATUMBULIWA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga,imemuachisha nafasi ya uongozi Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini Jonathan Agustino Madete kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Shinyanga Richard Masele, amebainisha hayo leo Juni 13,2024 wakati akitoa taarifa ya maamuzi ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama hicho.
“Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Mabala Mlolwa, kilichoketi leo, pamoja na mambo mengine kimemuachisha nafasi ya uongozi ndugu Jonathani Agustino Madete Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini kwa sababu ya utovu wa nidhamu,”amesema Masele.

Aidha, amesema vilevile Halmashauri Kuu imeazimia kwamwe haitamfumbia Macho wala kumvumilia Mtu yeyote awe kiongozi au Mwanachama wa CCM, atakayevunja kanuni,taratibu na Katiba ya Chama hicho, kwamba hatua za kinidhamu zitachukuliwa mara moja dhidi yake.
Amesema hiyo sababu ya kulinda heshima ya Chama na Jumuiya zake, ili kuhakikisha Misingi ya Chama na Miongozo inaendelea kuheshimiwa chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ni Mahiri, Mchapakazi, na Mazalendo wa kweli Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Jonatha Agustino Madete aliyetumbuliwa Uenyekiti UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Post a Comment

0 Comments