CHADEMA YAFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA SHINYANGA,YAHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA MPIGA KURA


CHADEMA YAFANA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA SHINYANGA,YAHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA MPIGA KURA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi.

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Shinyanga Mjini, kimefanya Mkutano wa hadhara na kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mkazi, pamoja na daftari la kudumu la Mpiga kura, ili wapate fursa ya kupiga kura kwenye chaguzi zijazo na kupata viongozi wenye kupigania maslahi yao, huku wakionyesha kusikitishwa Walengwa wa TASAF kulimishwa Mabarabara.

Mkutano huo wa hadhara umefanyika leo Juni 14,2024 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Town Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa Chama hicho pamoja na Mamia ya wananchi wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi akizungumza kwenye Mkutano huo, amewataka wananchi pindi uboreshaji wa daftari la kudumu la Mpiga kura litakapo anza wajitokeze kwa wingi kujiandikisha pamoja na daftari la Makazi, ili wapate fursa ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu mwakani (2025) na kupata viongozi sahihi.

“Wananchi wa Shinyanga ili mpate viongozi sahihi wenye kupigania maslahi yenu, lazima mjitokeze kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi, na mjiandikishe mapema kwenye daftari la Mkazi na daftari la kudumu la mpiga kura, ili mpate fursa ya kuchagua viongozi mnaowataka na siyo wakuchaguliwa ,”amesema Ntobi.
Katibu wa CHADEMA Aghata Mamuya.

“Nampige kura kwa kuchagua Mtu na siyo Chama na kuna Uongo ambao unazushwa kwamba mkichagua wapinzani hamuwezi kupata Maendeleo, niwapeni tu mfano mimi nilipokuwa Diwani wa Ngokolo mbona nilipata Lami na sasa Ngokolo ina Lami, na zile Kata za CCM hakuna Lami, ikiwamo Kata ya Kambarage,”ameongeza Ntobi.

Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Shinyanga Mjini Hamisi Ngunila, amewataka wananchi wa Shinyanga kwamba kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika mwaka huu, kwamba wasije wakafanya makosa, bali wachague viongozi makini wenye machungu na Taifa lao, na hivyo hivyo na katika uchaguzi Mkuu mwakani.
Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Hamisi Ngunila.

Amesema katika uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika mwaka huu,wataweka wagombea katika ngazi zote, na wagombea wao ni wale ambao wapo kwa ajili ya maslahi ya wananchi, na siyo kujali matumbo yao ambapo pia watakuwa wakisomea wananchi mapato na matumizi.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Shinyanga Agatha Mamuya, naye akizungumza kwenye Mkutano huo wa hadhara, ameonyesha kusikitishwa na kitendo cha Walengwa wa TASAF kulimishwa Mabarabara kwa Majembe ya Mikono ndipo walipwe pesa, huku akidai Walengwa wengine hadi sasa wanadai pesa za kulimishwa Mabarabara hayo.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Chadema.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464