MBIO ZA RUN FOR SIGHT "MARATHON" ZAWANUFAISHA WANANCHI SHINYANGA WAPATIWA HUDUMA YA MATIBABU BURE YA MACHO

MBIO ZA RUN FOR SIGHT "MARATHON" ZAWANUFAISHA WANANCHI SHINYANGA WAPATIWA HUDUMA YA MATIBABU BURE YA MACHO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Mkurugenzi wa Taasisi ya Majey Smart Vision Dk.Majala Majala.

TAASISI ya Majey Smart Vision kwa ufadhili wa Mbio za Run For Sight Marathon, imetoa huduma ya matibabu ya Macho bure kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga.

Huduma hiyo ya Matibabu bure ya Macho, ilianza kutolewa jana katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga ambayo itahitimishwa kesho.
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dk. Majala Majala ambaye pia ni Daktari wa Bingwa wa Macho, akizungumza na Waandishi wa habari leo Juni 18,2024, amesema wananchi wengi wamejitokeza kupata huduma hiyo ya Matibabu ya Macho.

Amesema jana waliona Wagonjwa wa Nje 857 na waliowafanyia upasuaji wa Macho ni 86, na kwamba huduma hizo zinatolewa bure chini ya Wafadhili Run For Sight Marathon, Lions Club na Rotary.
“Huduma hizi za Macho zinatolewa bure ambapo wananchi wenye shida kubwa watafanyiwa upasuaji, kupewa dawa na Miwani, na zoezi hili tuna hitimisha kesho baada ya hapa tuna kwenda Tabora,”amesema Dk.Majala.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dk.Elisha Robert, amesema zoezi hilo linakwenda vizuri, na kutoa wito kwa wananchi wa Shinyanga, wajitokeze kwa wingi kupata huduma hizo za Matibabu ya Macho bure kutoka kwa Madaktari Bingwa.
Nao baadhi ya wananchi wa Shinyanga akiwamo Mariamu Zacharia, ameshukuru kupewa huduma hizo za matibabu ya Macho bure na kuimarisha afya zao.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkurugenzi wa Taasisi ya Majey Smart Vision Dk. Majala Majala.akiangalia wagonjwa wa Macho ambao aliwafanyika upasuaji jana.
Wananchi wa Shinyanga wakiwa wamejitokeza kupata huduma ya Matibabu ya Macho bure.
Baadhi ya Wananchi wakiwa wamefanyiwa upasuaji wa Macho.
Baadhi ya Wananchi wakiwa wamefanyiwa upasuaji wa Macho.
Baadhi ya Wananchi wakiwa wamefanyiwa upasuaji wa Macho.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464