WEADO WASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA MTOTO WA AFRIKA SHINYANGA

WEADO WASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA MTOTO WA AFRIKA SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
SHIRIKA la Women Elderly Advocancy and Development Organization (WEADO),wameshiriki Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yamefanyika Kimkoa wa Shinyanga Kata ya Didia wilayani Shinyanga,huku watoto wakilaani kifo cha kikatili cha Mtoto mwenzao mwenye Ualbino Asimwe Novart (2)aliyeuawa kikatili.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Juni 19,2024 katika shule ya Msingi Didia wilayani Shinyanga,na kuhudhuliwa na Watoto,Wazazi,viongozi wa Serikali,na wadau mbalimbali wa Maendeleo,ambayo hufanyika kila mwaka Juni 16.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Mkoa wa Shinyanga Noelina Nicolaus, akizungumza kwenye Maadhimisho hayo,amewataka Wazazi kuacha kuwafanyia ukatili watoto na kuwatimizia mahitaji yao yote wakiwamo na watoto wenye ulemavu na kutowabagua.

Amewasihi pia wazazi kuendeleza vipaji vya watoto wao ili wapate ujuzi na hata wanapofikia hatua ya utu uzima wapate kujiajiri wenyewe.
Ametoa pia wito kwa watoto wenzao, kwamba wawe na maadili mema na kuwasilikiza wazazi wao na kutojiingiza kwenye makundi mabaya na kusababisha Mmomonyoko wa maadili.

Aidha,ameiomba Serikali kuendelea kuwachukulia hatua kali watu ambao wamekuwa wakiwafanyia watoto vitendo vya ukatili wakiwamo na wale ambao wamesababisha mauaji ya Mtoto mwenye Ualbino Asime Novert huko mkoani Kagera.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto wilaya ya Shinyanga Amina Hamisi, amewasihi watoto kwamba wanapokuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili wasikae kimya, bali wapaze sauti ili wahusika wachukuliwe hatua na kukomesha vitendo hivyo.

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Rehema Edson,ameitaka jamii,Mashirika, viongozi wa dini na Serikali,kuungana kwa pamoja kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na kutekeleza mahitaji yao.
Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko,akizugumza kwenye Maadhimisho hayo, ameiomba Jamii kuendelea kulinda haki za Mtoto,pamoja na wazazi kuhakikisha watoto wanakuwa na maadili mema.

Kwa upande wa Serikali,ameiomba kuendelea kusimamia sheria na kuwachukulia hatua kali wale watu ambao wamekuwa wakiwafanyia watoto vitendo vya ukatili na haki ipatikane.
Pia,katika Maadhimisho hayo kumefanyika Mdahalo juu ya Mada ya kupinga ukatili wa Kijinsia dhidi ya Watoto pamoja na Mada ya Maadili.

Kauli Mbiu katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika inasema"Elimu Jumuishi kwa watoto izingatie Maarifa,Maadili na Stadi za Kazi."

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Rehema Edson akizungumza kwenye madhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Mkoa wa Shinyanga Noelina Nicolaus, akizungumza kwenye Maadhimisho hayo ya Siku ya Mtoto Afrika.
Mwenyekiti wa Baraza la Watoto wilaya ya Shinyanga Amina Hamisi akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya Siku ya Mtoto Afrika.
Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko (katikati)akiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Kimkoa mkoani Shinyanga.
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mkoani Shinyanga yakiendelea.

Mtoto Neema Jacob akipewa fedha kwa ajili ya kununua Begi la Shule na Viatu.
Watoto kutoka Shirika la WEADO wakishiriki Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mkoani Shinyanga.

Picha ya pamoja ikipigwa.

Picha ya pamoja ikipigwa
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464