Na Marco Maduhu,SHINYANGA
DC Mtatiro.
MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro,amewasilisha Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, ya mwaka 2020/2025 kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni 2024.
Amewasilisha
taarifa hiyo leo Juni 20,2024 kwenye Kikao Maalum Cha Halmashauri Kuu ya CCM
Wilaya ya Shinyanga Mjini.
Amesema kwa
kipindi hicho Rais Samia ametoa fedha nyingi Zaidi ya Bilioni 35.6, ambazo
zimetekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa wananchi. na kuitekelezaji
Ilani ya CCM kwa asilimia 100.
Uwezeshaji wananchi kiuchumi
Akielezea eneo
la Uwezashaji wananchi kiuchumi, amesema Serikali chini ya Rais Dk.Samia Suluhu
Hassan, imeendelea kutoa fedha kwa Walengwa wa TASAF na kuzinusuru Kaya
Maskini, pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kurudisha Mikopo ya Halmashauri
asilimia 10.
Miundombinu ya Barabara
Amesema Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA)Tayari wameshapokea kiasi cha fedha Sh.Milioni 853 kwa ajili ya uboreshaji wa Miundombinu ya barabara.
“Hapa kwenye
Barabara napenda kuzungumza kidogo kuna Miradi 10 ambayo inaendelea ya ujenzi
wa Barabara, lakini iliyokamilika ni Miradi 4, na Miradi 6 bado haijakamilika,
na Miradi hii 6 ipo ndani ya uwezo wangu, Wakandarasi wajipange wapo ambao
tutavunja Mikataba, kuwakamata,na kuzuia wasifanye kazi tena hapa
Shinyanga,”amesema Mtatiro.
Maji
Amesema kwa
maeneo ambayo bado hajafikiwa na huduma ya Maji, Mikataba mbalimbali imesainiwa
na wapata pata huduma hiyo.
Umeme
Amesema kazi ya
kusambaza ya umeme inaendelea na wananchi wengi wameshafikiwa na huduma hiyo.
Afya.
Amesema huduma
za Afya zinaendelea kuboreshwa na Rais Samia, na hivi karibuni ametoa fedha katika
Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Zaidi ya Sh.bilioni 1, na ukarabati wa
Majengo unaendelea.
“Rais Samia pamoja na wasaidizi wake akiwamo
na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,amekuwa wakifanya kazi
kubwa sana kwenye Sekta ya Afya, tunaona mambo makubwa ambayo yanafanyika,
tuendee kuwa unga mkono na kuwatia Moyo hawa viongozi wetu,”amesema Mtatiro.
Elimu
Amesema fedha zimeendelea kutolewa kwenye Sekta ya Elimu, zikiwamo za Elimu bure, pamoja na kuboresha miundombinu ya Sekta hiyo zikiwamo Maabara za Sayansi na wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki.
Mwenyekiti wa
CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe, akizungumza kwenye kikao
hicho,amempongeza Rais Samia kwa kuitekeleza ilani ya CCM kwa asilimia 100 na
kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo ikiwamo ya kimkakati.
Katibu wa CCM
Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo naye ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais
Samia, pamoja na wasaidizi wake kwa kazi kubwa ambayo anaifanya, wakiwamo na
Watumishi wa Serikali kwa kusimamia miradi ya maendeleo vizuri na kuzitendea
haki fedha ambazo zinatolewa na Rais.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇