Header Ads Widget

RIPOTI; WAANDISHI WA HABARI WA MAZINGIRA NA HALI YA HEWA WAKABILIWA NA UKOSEFU WA RASILIMALI NA VITISHO


Ripoti: Waandishi wa Habari wa Mazingira na Hali ya Hewa Wakabiliwa na Ukosefu wa Rasilimali na Vitisho
Na Mwandishi Wetu

Ripoti ya hivi karibuni ya Internews, iliyofanywa kupitia mpango wake wa Uandishi wa Habari za mazingira kupitia shirika lake la Earth Journalism, imetoa tathimini ya kina kuhusu hali ya uandishi wa habari za hali ya hewa na mazingira duniani. Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi chache zilizojumuishwa katika utafiti huu wa kimataifa, ikitoa maarifa muhimu kuhusu mitazamo na uzoefu wa Waandishi wa habari katika eneo hilo.

Matokeo yanaonyesha kuwa kwa Tanzania nanchi nyingine uandishi wa habari za mabadiliko ya hali ya hewa na masuala ya mazingira umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Kuongezeka kwa habari hizi kunahusishwa hasa na matatizo ya mazingira yanayozidi kuongezeka na, kwa kiwango kidogo, kuongezeka kwa hamu ya jamii kufhamu kuhusu masuala haya muhimu ya mazingira.

Ripoti hiyo inaonyesha kwamba Asilimia 82 ya waandishi wa habari duniani kote walikubali kuwa habari za hali ya hewa na mazingira kwasasa zina umuhimu zaidi ikilinganishwa na miaka kumi oiliyopita..

Hata hivyo, licha ya ongezeko hilo ripoti hiyo inaonyesha kwamba waandishi wa habari wanakubali kwamba habari za mazingira wanazoripoti hazitoshi ukilinganisha na uzito au ukubwa la mabadiriko ya tabia nchi na hali ya hewa.

Ripoti imeonyesha kwamba waandishi wengi wanaandika habari za hali ya hewa na mazingira kwa kuangalia Zaidi katika mtazamo wa afya (asilimia 70), wakisisitiza uhusiano kati ya uharibifu wa mazingira na afya ya jamii Mada nyingine zilizopewa kipaumbele mara nyingi ni pamoja na ukataji miti (asilimia 58), maji na usafi wa mazingira (asilimia 58), uchafuzi wa maji (asilimia 57), sera za serikali (asilimia 56), na uchafuzi wa plastiki (asilimia 53).

Pamoja na mafanikio hayo ripoti hiyo imeonyesha changamoto kadhaa zinazowakabili waandishi wa habari wanaondika masuala ya hali ya hewa na mazingira. Asilimia 76 kubwa ya waandishi wa habari walitaja ukosefu wa rasilimali kama kikwazo kikubwa. Aidha, dhana ya "usawa" bado ipo, ambapo asilimia 62 ya waandishi wa habari waliohojiwa wanajumuisha vyanzo vya habari vya

Kanuni za kitaaluma kama vile mlengo wa habari zinaendelea kuwa msingi kwa waandishi wengi wa habari, huku wachache wakitetea misimamo au sera maalum. Kwa kushangaza, asilimia 39 ya waandishi wa habari waliripoti kutishiwa au kujizuia kuandika habari zinazohusu masuala ya hali ya hewa na mazingira, huku vitisho vikijitokeza zaidi kutoka kwa watu wanaofanya shughuli haramu zinazohusiana na mazingira.

Taarifa za kupotosha ni changamoto kubwa kwa uandishi wa habari za hali ya hewa na mazingira. Kulingana na ripoti hiyo, asilimia 58 ya waandishi wa habari waliona ongezeko la taarifa za kupotosha katika muongo uliopita, ambazo zinasambazwa zaidi kupitia mitandao ya kijamii. Taarifa hizi za kupotosha zinadhoofisha uelewa wa umma kuhusu masuala ya hali ya hewa, ambapo asilimia 90 ya waandishi wa habari walikubali athari zake mbaya kwenye habari zao.

Ili kushughulikia changamoto hizi, ripoti inapendekeza mashirika ya ndani na kimataifa kuongeza msaada kwa waandishi wa habari wanaofunika mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira na kushirikiana na waandishi wa habari na vyumba vya habari ili kuhakikisha ufadhili ulioelekezwa na endelevu.

Ripoti imependekeza pia kwamba waandishi wa habari walenge katika kuandika masuala ya kimataifa ya mazingira kwa kuyalinganisha na maeneo yao huku wakiepuka kutoa nafasi kwa watu au taasisi zinazopinga mabadiriko ya hali ya hewa.

Ripoti pia inapendekeza vyumba vya habari na wahariri kuhamasisha waandishi wa habari kubobea katika uandishi wa habari za hali ya hewa na mazingira huku wakitoa kipaumbele katika kuchapisha na kutangaza habari za hali ya hewa na mazingira mara kwa mara.

Post a Comment

0 Comments