RC MACHA ATOA ANGALIZO HALMASHAURI YA KISHAPU KUPATA HATI SAFI KWA KUJIBU HOJA ZA CAG
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani humo kwa kupata Hati Safi, kutokana na kujibu Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa Fedha (2022/2023) unaoishia Juni 30, huku akitoa angalizo kwamba Hati hiyo isiwaleweshe Sifa bali iwatie Moyo na kuendelea kufanya kazi kwa bidii.
Amebainisha hayo leo Juni 24,2023 kwenye Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu,cha kujadili utekelezaji wa Maagizo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha (2022/2023) unaoishia Juni 30.
Amesema anawapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kupata Hati Safi, na kueleza kuwa wamepata Hati hiyo kwa kielelezo kwamba wamezingatia taratibu zote za Kihasibu, lakini siyo utekelezaji wa Majukumu umekamilika kama inavyotakiwa, na kubainisha kwamba Hati hiyo Safi isije kuwalewesha bali iwatie moyo na kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kufuata taratibu zote za Utumishi.
“Nawapongeza Halmashauri ya Kishapu kwa kupata Hati Safi kwa kujibu Hoja za CAG, lakini hoja zingine zinatokana na kukosa “U-Seriousness” wa kufanya kazi,”Amesema Macha.
“Kwa zile hoja ambazo zipo kwenye hatua ya utekelezaji zifanyiwe kazi haraka sana, likiwamo hili la ukosefu wa Hati Miliki za Ardhi 213 kwamba zilizopatikana ni Nne tu, na upelekaji Makato ya Mishahara ya Watumishi kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii PSPF,”Ameongeza Macha.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson, amesema zamani Halmashauri hiyo ilikuwa kwenye nafasi ya 10 bora ya Halmashauri hapa nchini yenye hoja nyingi za CAG, lakini sasa hivi haina hoja hizo, na kasi waliyonayo watakwenda kuingia kwenye 10 bora ya Halmashauri ambayo haitakuwa na hoja nyingi.
Naye Mwekahazina wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Geogre Sulumbwe, akiwasilisha taarifa ya cha utekelezaji wa maagizo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kwa mwaka wa fedha 2022/2023 unaoishia Juni 30, amesema walikuwa na hoja 35, Saba zimefungwa, 27 zipo kwenye hatua ya utekelezaji, na Moja bado haijatekelezwa na wamepata Hati Safi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani Kishapu cha kujadili Hoja za CAG.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Wiliamu Jijimya akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani Kishapu cha kujadili Hoja za CAG.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha kuajdili Hoja za CAG.
Mwekahazina wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Geogre Sulumbwe wakiwasilisha taarifa ya CAG kwenye Baraza la Madiwani Kishapu cha kujadili Hoja za CAG.
Viongozi wakiwa Meza kuu kwenye Baraza hilo.
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakiwa kwenye Kikao Maalumu cha kujadili Hoja za CAG.
Kikao cha Baraza kikiendelea.
Kikao cha Baraza kikiendelea.
Kikao cha Baraza kikiendelea.
Kikao cha Baraza kikiendelea.
Kikao cha Baraza kikiendelea.
Kikao cha Baraza kikiendelea.
Kikao cha Baraza kikiendelea.
Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.
Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.
Kikao cha Baraza la Madiwani kikiendelea.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464