Header Ads Widget

RC MACHA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA KUPATA HATI SAFI



Na Mapuli Kitina Misalaba

Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imepata hati safi kutokana na kujibu hoja za mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) kwa Mwaka wa fedha 2022/2023.

Hayo yamebainishwa leo kwenye Kikao cha Baraza Maalum cha Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kilichojadili taarifa za utekelezaji wa majibu ya hoja zao Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG.

Akiwasilisha taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa hesabu zilizokaguliwa katika Mwaka unaoishia terehe 30 Juni, 2023 Mweka hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bwana Thobias Shija ameitaja Halmashauri hiyo kupata hati safi.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ametumia nafasi hiyo kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa kupata Hati Safi, huku akisisitiza kutoridhika na hati safi hiyo ambapo amewahimiza kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa juhudi na ushirikiano uliopo ili kuendeleza matokeo chanya ya kimaendeleo.

Amewataka watendaji wa halmashauri kuwajibikia majukumu yao kila mmoja kulingana na nafasi yake ili kwa pamoja waweze kuleta tija na ufanisi na kuchochea maendeleo



Amewataka Madiwani kupitia mikutano yao ya hadhara kuwaelimisha na kuhamasisha wananchi kujiunga na Bima ya Afya ili waweze kujikwamua kiafya.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nikodemus Luhende amesema Halmashauri hiyo kupitia madiwani, wataendelea kushirikiana na wataalam mbalimbali katika kuleta maendeleo zaidi kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kupata hati safi.










Post a Comment

0 Comments