Header Ads Widget

DC MTATIRO AWAOMBA WADAU WA MICHEZO KUWEKEZA NGUVU PIA KWENYE MPIRA WA WAVU

DC MTATIRO AWAOMBA WADAU WA MICHEZO KUWEKEZA NGUVU PIA KWENYE MPIRA WA WAVU

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro,amewaomba Wadau wa Michezo kwamba wanapowekeza nguvu kwenye Michezo Mingine waukumbuke pia na Mpira wa Wavu,ili kuuinua Mchezo huo na kutoa Ajira kwa Vijana.

Amebainisha hayo leo Juni 29,2024 wakati akifungua Mashindano ya Mpira wa Wavu Ligi ya Kanda ya Ziwa Magharibi ambayo inashirikisha Timu Nne ili kupata Washindi wawili ambao watakwenda kuwakilisha Ligi ya Mpira wa Wavu Tanzania Julai 22 Mwembe Yanga Jijini Dar es Salaam.
Amesema anakipongeza Chama Cha Mpira wa Wavu Tanzania kwa kuendeleza Mpira huo wa Wavu, ambao ni fursa ya Ajira kwa vijana na kuwaomba Wadau mbalimbali wa Michezo kwamba wanapokuwa wakiwekeza nguvu kwenye Michezo mingine waukumbuke pia na Mpira wa Wavu.

“Natoa Wito kwa wadau mbalimbali wa Michezo hapa nchini wanapowekeza nguvu kwenye Michezo Mingine, wakumbuke pia na kuwekeza nguvu kwenye Mpira wa Wavu sababu ni fursa pia kwa vijana kupata Ajira,”amesema Mtatiro.
Katibu wa Chama Cha Mpira wa Wavu Tanzania Laurence Safari, amesema Ligi hiyo ya Kanda ya Ziwa Magharibi inashirikisha Timu Nne kutoka Kigoma,Tabora, Simiyu na Kahama, na kwamba Timu mbili zitakazoshinda ndiyo zitakwenda kuwakilisha Ligi ya Mpira wa Wavu Tanzania(Tanzania Valleball National League) Julai 22 Jijini Dar es Salaam.

Amesema Ligi hiyo ya Mpira wa Wavu Taifa itashirikisha Vilabu 24, vya wanaume 14 na wanawake 10, na Washindi Watatu watakwenda kuwakilisha Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika mwakani.
Naye Mwenyekiti wa Mpira wa Wavu Kanda ya Magharibi Jason Rwekaza, amesema katika Ligi hiyo ya Kanda ambayo inachezwa leo mkoani Shinyanga kwamba Mshindi wa kwanza atakayepatikana anapewa zawadi ya Kombe.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza na Wachezaji wa Mpira wa Wavu.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akifungua Mashindano ya Mpira wa Wavu Kanda ya Ziwa Magharibi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro(kushoto)akiteta Jambo na Katibu wa Chama Cha Mpira wa Wavu Tanzania Laurence Safari.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro (kushoto) akiteta Jambo na Katibu wa Chama Cha Mpira wa Wavu Tanzania Laurence Safari.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro (kushoto)akiangalia Mpira wa Wavu na Katibu wa Chama Cha Mpira wa Wavu Tanzania Laurence Safari.
Ligi ya Mpira wa Wavu Kanda ya Ziwa Magharibi ikiendelea.

Post a Comment

0 Comments