Header Ads Widget

WATOTO KANISA LA IEAGT SHINYANGA WALAANI MAUAJI YA MTOTO MWENYE UALBINO ASIMWE NOVATH WAKIADHIMISHA WIKI YA WATOTO KANISANI HAPO

WATOTO KANISA LA IEAGT SHINYANGA WALAANI MAUAJI YA MTOTO MWENYE UALBINO ASIMWE NOVATH WAKIADHIMISHA WIKI YA WATOTO KANISANI HAPO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
WATOTO katika Kanisa la International Evengelical Assemblies Of God Tanzania (IEAGT)Kambi ya Waebrania Mjini Shinyanga,wamelaani Mauaji ya Mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novath(2) ambaye aliuawa kikatili kwa kukatwa viungo vyake mkoani Kagera,huku wakiipongeza Serikali kwa kuchukua hatua na kuwakamata watu wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo.

Wamelaani mauaji hayo leo Juni 30,2024 katika Ibada ya kuhitimisha wiki ya Watoto Kanisani hapo, iliyoanza Juni 23 ikiwa na Malengo ya kuwapatia Watoto Mafundisho ya Kiroho na Kimwili huku wakiongozwa na Neno kutoka Mithali 22;6 lisemalo “Mlee Mtoto katika Njia impasayo, Naye hataiacha hata atakapokuwa Mzee”.
Akisoma Risala kwa Niaba ya Watoto wenzake Ibrahim Jacob,amesema hali ya ulinzi kwa watoto imekuwa haiwapi Amani, na kulaani Mauaji ya Mtoto mwezao mwenye Ualbino Asimwe Novath, ambaye aliuawa kikatili kwa kukatwa viungo vyake huko Kagera.

"Watoto katika Kanisa letu la (IEAGT) tuna laani Mauaji ya Mtoto mwenzetu Mwenye Ualbino Asimwe Novath aliyeuawa kikatili huko Kagera kwa kukatwa viungo vyake," amesema Ibrahim.
Aidha,amesema wanapinga vitendo vyote vya ukatili ambavyo wamekuwa wakifanyiwa watoto vikiwamo vipigo,ubakaji, ulawiti,utekelezaji,lugha za matusi pamoja na kuozeshwa ndoa za utotoni na kukatishwa masomo.

Wamewaomba pia wazazi na walezi kuwalea watoto katika njia ipasavyo ikiwamo ya Kiroho, pamoja na kuwaruhusu kuhudhuria kwenye mafundisho mbalimbali ya neno la Mungu ili wapate Mibaraka na kuwa na Maadili Mema.
Katika hatua nyingine wamewaomba wazazi washirikia kikamilifu kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika mwaka huu, na kwamba wasije wakaingiwa na Ibirisi na kusababisha vurugu kwenye uchaguzi huo,bali uwe na Amani na Utulivu.

Awali Mtoto David Lameck akitoa Mahubiri kwenye Ibada hiyo, ametoa wito kwa Watoto na Watu wazima kwamba wanapokuwa katika Madhabahu pa bwana,wanapaswa kuwa na heshima ili wampate Mungu.
Askofu wa Kanisa hilo David Mabushi,amesema Risala hiyo ya watoto imewagusa kutokana na kuonyesha wasiwasi wao juu ya hali ya usalama wao,na kuwasihi Wazazi kuwajibika kuwalinda Watoto bali wasiwatelekeze, hadi watakapofika hatua ya kujitegemea.

"Tunapoona mauaji yanayoendelea leo siyo jambo la kawaida, Mtoto Asimwe ameuawa kwa ushirikiano wa mzazi wake ambaye alipaswa kumlinda, lakini kwa taama ya pesa akamuuza mwanawe kitendo ambacho niche kikatili sana," amesema Askofu Mabushi.
Aidha, amesema kwa mauaji hayo ya Mtoto Asimwe, kwamba Kanisa hilo linaungana na Serikali kupinga ukatili wa aina yoyote ule hapa nchini.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Askofu wa Kanisa la IEAGT David Mabushi akizungumza kwenye Ibada ya Wiki ya Watoto Kanisani hapo.
Askofu wa Kanisa la IEAGT David Mabushi akiwa na Mkewake kwenye Ibada ya wiki ya Watoto Kanisani hapo
Mlezi Mkuu wa Watoto Kanisa la IEAGT Estomane Henry akizungumza kwenye Ibada ya wiki ya Watoto Kanisani hapo.
Mtoto Ibrahim Jacob akisoma Risala kwa Niaba ya Watoto wenzake.
Mtoto David Lameck akitoa Mahubiri kwenye Ibada hiyo.
Mtoto David Lameck akiendelea kutoa Mahubiri.
Watoto wakisoma Maandiko ya Neno la Mungu katika Biblia.
Watoto wakisoma Maandiko ya Neno la Mungu katika Biblia.
Watoto wakisoma Maandiko ya Neno la Mungu katika Biblia.
Watoto wakisoma Maandiko ya Neno la Mungu katika Biblia.
Watoto wakiendelea na Ibada.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Waumini wa Kanisa la IEAGT wakiwa kwenye Ibada ambayo inaendeshwa na Watoto wao.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Viongozi wa Kanisa la IEAGT wakiendelea na Ibada ambayo inaongozwa na Watoto.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Ibada ikiendelea.
Watoto wakiimba Nyimbo za Kumsifu Bwana.
Watoto wakiendelea kuimba Nyimbo za Bwana.
Nyimbo zikiendelea kuimbwa.
Nyimbo zikiendelea kuimbwa.
Nyimbo zikiendelea kuimbwa.
Awali watoto wakiwa katika Maandamano huku akibeba Mabango ya kupinga Vitendo vya Ukatili dhidi yao pamoja na kulaani Mauaji ya Mtoto Mwenye Ualbino Asimwe Novath aliyeuawa kikatili huko Kagera.
Mtoto mwenye Ualbino akiwa amebeba Picha ya Mtoto Mwezake Mwenye Ualbino Asimwe Novath ambaye aliuawa kikatili huko Kagera akilaani Mauaji hayo.
Watoto wakiwa katika Maandamano huku akibeba Mabango ya kupinga Vitendo vya Ukatili dhidi yao pamoja na kulaani Mauaji ya Mtoto Mwenye Ualbino Asimwe Novath aliyeuawa kikatili huko Kagera.
Watoto wakiwa katika Maandamano huku akibeba Mabango ya kupinga Vitendo vya Ukatili dhidi yao pamoja na kulaani Mauaji ya Mtoto Mwenye Ualbino Asimwe Novath aliyeuawa kikatili huko Kagera.
Watoto wakiwa katika Maandamano huku akibeba Mabango ya kupinga Vitendo vya Ukatili dhidi yao pamoja na kulaani Mauaji ya Mtoto Mwenye Ualbino Asimwe Novath aliyeuawa kikatili huko Kagera.
Mtoto mwenye Ualbino Agnes Kabika akiwa amebeba Picha ya Mtoto Mwezake Mwenye Ualbino Asimwe Novath ambaye aliuawa kikatili huko Kagera akilaani Mauaji hayo.
Watoto wa Kanisa la IEAGT wakiwa wamebeba Picha ya Mtoto Mwenye Ualbino Asimwe Novath na kulaani Mauaji hayo ya Mtoto mwenzao.
Watoto wa Kanisa la IEAGT wakilaani Mauaji ya Mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novath aliyeuawa kikatili huko Kagera.
Muonekano wa Kanisa la IEAGT ambalo linaungana na Serikali kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto pamoja na kulaani Mauaji ya Mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novath aliyeuawa kikatili huko Kagera kwa kukatwa viungo vyake.

Post a Comment

0 Comments